Farid Mussa afaulu majaribio Hispania

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
FARID MUSSA AFAULU MAJARIBIO HISPANIA, DEPORTIVO TENERIFE WAJA MEZANI AZAM FC



Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam

WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Farid Mussa Malik (pichani kulia) wa klabu ya Azam ya Dar es Salaam amefaulu majaribio katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania.

Mkurugenzi wa Azam FC, Yussuf Bakhresa anayefuatilia majaribio ya mchezaji huyo Hispania, ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba CD Tenerife sasa inatarajiwa kuingia katika mazungumzo na Azam FC juu ya kumnunua mchezaji huyo.

“Tunatarajia kuanza mazungumzo nao juu ya suala la Farid, ingawa wazo lao la awali ni kumchukua kwa mkopo wa miaka miwili. Sasa tunasubiri ofa yao rasmi, kisha Bodi ya Ukurugenzi itajadili na kutoa maamuzi,”amesema Bakhresa.

Kwa upande wake, Farid amefurahia matokeo hayo na kusema haikuwa kazi nyepesi kwake kuweza kuwaridhisha maofisa wa benchi la ufundi la Tenerife.





“Kwa kweli nimefurahi sana na ninamshukuru Mungu kwa kufuzu majaribio, ila haikuwa kazi nyepesi, mpira wa Ulaya mgumu,”amesema.

Awali, Farid ilikuwa apelekwe moja ya klabu za Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga, kati ya Las Palmas na Athletic ya Bilbao kwa majaribio, lakini wakala wake akashauri mchezaji huyo aanzie timu ya Daraja la Kwanza Hispania ili kupata nafasi ya kucheza na kuinuka haraka.
 
Tumechoshwa na porojo hebu tumwone kwenye kioo kwanza tuhakikishe wenyewe
 
Azam wamruhusu tu hata kwa mkopo.
Hata kwa mwaka mmoja.
Hivi Ngasa na Msuva wako wapi?

Kuna yule mwashiuya,bado yupo hapo kwa Snura?
 
Shida huongeza uwezo wa kufikiri na kujituma.So usishangae wachezaji wote wazuri kutokea uswazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…