Wakati fulani tuliwahi kucheza mechi ya kirafiki
kama taifa (Taifa Stars) na tulicheza na taifa
kubwa katika soka Duniani, Brazil wakati ule
tuliambiwa Tanzania ni nchi ya TATU
ulimwenguni kwa kuwa na vipaji halisi vya soka
(watu wanazaliwa na vipaji hivyo hawafundishwi
popote) katika orodha ile ipo Brazil,Nigeria &
Tanzania.... sijui kama ni kweli.!!
Tafakari yangu inanifanya niamini katika hilo toka
kizazi cha akina Kibadeni,Tenga,Mkwasa,Manara
njoo katika zama za akina Mwameja,Lunyami
la,Mohamed Hussein,Amlima,Kenny Mkapa je
kuhusu akina Ali Mayai,Pawasa na wengineo??
inawezekana kweli si ndiyo?? Ndiyo sisi tuna
vipaji vingi sanaaaaa...!!
Nenda Songea,Mwanza,Mtwara,Lindi,Musoma
sijui wapi utawakuta watu wamejariliwa kweli
kweli, lakini nini kinatuangusha? Mfumo?
Uongozi,hulka yetu ya Simba na Yanga? malezi?
au?? inasikitisha sana kuona mpaka sasa hatuna
wachezaji walau wa5 wanaocheza nje ya nchi,
ndiyo inauma sanaaaa..!!
Ujio wa klabu ya Azam nadhani umeongeza wigo
wa kuwaona vijana wengi wenye vipaji, panapo
majaliwa,kijana Farid anapanda ndege kuelekea
Hispania miongoni mwa nchi zilizo na ligi bora na
maendeleo ya kweli katika ulimwengu wa soka,
tumuombe afanikiwe tuwe na wachezaji wengi
wanaocheza nje ambao wataleta uzoefu katika
timu yetu ya Taifa,Taifa Stars, ndiyo tufanye
hivyo kwa faida ya maendeleo ya nchi yetu
kumbe tufanyaje??
Iko hivi kufanya vizuri kwa akina
Samata,Ulimwengu,Ngassa na sasa Farid sijui
ingekuwaje kama Haruna Moshi "Boban" kama
angeendelea kuwepo katika soka la Ulaya uwepo
wao kule utafungua milango kwa vijana wengi
ambao sasa wametambua kuwa soka ni ajira,
ndiyo ajira za maofisini siku hizi hakuna,kwa nini
wasitumie vipaji vyao?? huu ndiyo wakati wao.
Kama vipaji tunavyo tena vingi vya "kumwaga"
nini tunasubiri?? kwanza vyama vya michezo
hasa vinavyosimamia soka waelewe kuwa sasa
soka ni ajira tosha wawepo watu wa kweli wa
mpira siyo "wapiga dili" ieleweke kuwa upigaji
wao dili unaua soka letu, tupate mawakala wengi
na wa" ukweli" ambao watafungua milango ya
vijana wengi ambao wametapakaa kila kona ya
nchi hii makocha waendee huko vijijini vipaji vipo
vingi nani alikiwa anamjua yule dogo wa Yanga
Godfrey Mwashiuya?? bhaaa! hao wapo wengi
nawaambia nendeni huko msikalie tuu hapo
Karume mnapigwa na viyoyozi..cheee!!
Kuna kocha mmoja alikuwa wa Kameruni,yule
bwana mkubwa alifanya mashindano ya nchi
nzima tena vijijini huko akawaibua watu kama
akina Njitap,Kala Nkongo yule beki kisiki na
wengine wengi ambao wakapata kuonekana na
vilabu vya Kameruni mbona hakukaa pale Younde
kupiga mvinyo?? Watumieni wachezaji wa zamani
waliotapakaa kote nchini kuwa "maskauti" wa
vipaji vinavyoishia kunywa gongo na pombe za
kienyeji huko vijijini kwa wakazi wa Mtwara
mnamkumbuka jamaa mmoja alikuwa anaitwa
Mussa Kichawi?? alikuwa anakaa kule Magomeni
yupo wapi?? viongozi wa soka msaikae
maofisini.....!!
Mengi ningeandika kuhusu nafasi na kupotea kwa
vipaji vyetu vingi nichelee kusema nenda
Farid,kafanye kweli kwani hayo ndiyo maisha
yako,Mungu amekupa kipaji,kitumie, kipaji mtaji
Mungu akuongoze katika safari yako ya majaribio
Hispania tena nasikia unaenda La liga,si ndiyo
kule yupo Messi,C7,Suarez,Neymar na yule kocha
mwehu mwenye midadi? Simeone?? aaaah
kafanye kweli bwana nafasi ndiyo hii haiji mara
mbili...!!
Kila la heri Farid miongoni mwa vipaji vya kweli
vya soka vilivyochomoza miaka ya karibuni hapa
nchini.