Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Kagera Komredi Faris Buruhani ameendelea na Kampeni ya kuwanadi wagombea wa CCM katika mitaa mbalimbali ya Mkoa wa Kagera inaendelea katika Mitaa 10 ya Kata za Hamugembe, Miembeni, Bilele na Kashai Manispaa ya Bukoba.
"Hakika utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 umetosha kuwafanya wagombea wetu kuwa kivutio kikubwa mbele ya wananchi. Hivyo ushindi wa kimbunga wa Chama chetu Novemba 27 ni suala la muda tu" - Komredi Faris Buruhani
"Katika kila Kijiji, kila Mtaa, kila Kivuko na kila Kona ya Kagera, Chama Cha Mapinduzi (CCM) tunasimama imara kusaka ushindi kwa hoja za maendeleo na mshikamano wa kweli" - Komredi Faris Buruhani
#Siku7ZaKubebaKilaKitu
#PigaKuraJengaKitaa
#TunazimaZoooteTunawashaKijani