Fastjet cancellation zimezidi

Fastjet cancellation na Delay naona sasa imekuwa jadi aisee. Ndege ile ya Alfajiri ya kwenda KIA tokea DAR ES SALAAM imezidi delay lazima mfahamu kuwa tulipochagua hiyo ndege tuna safari ndefu ya kuunganisha mfano Tarehe 05.03 tulikuwa group tunaenda ADDIS sasa tulikuwa tunaunga 2 Nairobi then tukwee Ethiopian maana ni gharama sana kupanda Ethiopian kupandia DAR/KIA delay yenu ilitufanya tumiss flight NAIROBI.
 
Fastjet wanabidi wajipange haswa pamoja na kwamba wanaturahishia usafir kwa gharama nafuu lakini naona kama wanajisahau wakati mwingine. PW nao walianza kuota pembe wakati Fulani leo imebaki historia
 
hao wafanyakazi wao ndo balaa ukiongea kiingereza tu ndo umeloga, full kigugumizi
 
Fastjet nafikiri hawajipanga maana wameingia sokoni wakapata muitikio mzuri wa wateja baadae sasa wamezidiwa abiria lakini hawataki kuongeza ndege kilichobaki sasa ni kufanya cancellation za makusudi ili ku-accomodate ongezeko la abiria
 
Kwenda Mwanza 400000 return huu ni ukichaa ule ule
 
bei zao sasa ni kutupa aisee, halafu ndo delay kila kukicha daah hawa jamaa noma. ATCL fufuka hata leo basi tufurahie usafiri wa ndege
 
fastjet hata waki-cancel wao safari kuku-refund ile nauli yako ni ishu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…