Kwa mujibu wa matangazo hayo, ni kwamba baba mtu mzima/mwenye adhi/uwezo wa kifedha na ambaye anahisiwa kuwa muathirika wa ukimwi (tafsri yangu binafsi kutokana na ninavyolielewa tangazo hilo) anamlaghai mtoto mdogo kwa vizawadi vidogovidogo na chips ili akafanye naye tendo la ngono. Huyu ndiye anaitwa Fataki kwa mujibu wa tangazo hilo linalosikika kwenye vituo vya Redio takribani viwili.
Sasa swali langu ni kwamba, je, hakuna hakina mama wa aina hii ambao nao huwalaghai wavulana wadogo kwa kuwafadhili ktk masuala madogomadogo kwa lengo hilo hilo? Kama wapo, ni kwanini tangazo hili linakuwa selective?