Kuna tangazo ambalo linalenga kuwaepusha akina dada (hasa wale wenye umri mdogo) na uchu wa akina baba wapenda ngono. Binafsi sina tatizo sana na ujumbe uliomo kwenye matangazo haya, tatizo langu ni kwamba mbona wanaandamwa akina baba tu? Je, hakuna akina Mama ambao ni FATAKI??????
Naomba utu elimishe sisi tusio jua. Fataki ni nini hapa kwa unavyo maanisha wewe?
Kwa mujibu wa matangazo hayo, ni kwamba baba mtu mzima/mwenye adhi/uwezo wa kifedha na ambaye anahisiwa kuwa muathirika wa ukimwi (tafsri yangu binafsi kutokana na ninavyolielewa tangazo hilo) anamlaghai mtoto mdogo kwa vizawadi vidogovidogo na chips ili akafanye naye tendo la ngono. Huyu ndiye anaitwa Fataki kwa mujibu wa tangazo hilo linalosikika kwenye vituo vya Redio takribani viwili.
Sasa swali langu ni kwamba, je, hakuna hakina mama wa aina hii ambao nao huwalaghai wavulana wadogo kwa kuwafadhili ktk masuala madogomadogo kwa lengo hilo hilo? Kama wapo, ni kwanini tangazo hili linakuwa selective?
Mkuu heshima mbele. mambo ya haki sawa kwa wote uta gundua lina pigiwa bango tu kama huyo anaye nyimwa huyo haki ni mwanamke. Hiyo ndiyo hali halisi. Aki pendelewa mwanamke huto sikia mtu akisema chochote. Nadhani jamii ina bidi ijifunze kuwa haki sawa kwa wote ina maanisha haki sawa kwa wote.