Tausi Mzalendo;
Naheshimu mawazo na mchango wako.Ukiacha huko kujihami kwa kudhania wakati kuna namna nyingi za kujua kama mtoto ni wako ama la, je wanaume wanapomwadhibu mama hawaoni adhabu kubwa anaipata mtoto ambaye hakuomba mmsababishe kuja duniani/
Kwamba mama hakuwa mwaminifu, sidhani kunakuja kama kishtukizo.Mwanaume unapojamiiana na mwanamke bila kinga unategemea nini?
Maswala ya DNA kwenye ulimwengu wa tata kwani yameanza lini Tausi? Tofauti na DNA kuna njia ipi unayoweza kuthibitisha kama mtoto ni wako? Ni wakina mama wangapi wameolewa lakini wamebambika waume zao watoto wa wanaume wengine na wahusika hawajui?. Si wote wanaweza kumdu gharama za kwenda kupima DNA hasa huku bongo hivyo wahusika (wanaume wanakataa watoto) wakijuwa kuwa hawakuwa peke yao kimapenzi na mdada ndiyo maana wanakuwa wagumu kukubali mimba---mtoto kama watakuwa hawana uwakika wa kutosha. Hata kwenye hizo shows alizozitaja Mzee Mwanakijiji, sababu kubwa ya wababa kukataa watoto wao kama hawajapima DNA ni wadada kuwa na mahusiano na mtu zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Wakipima DNA na majibu yakasema watoto ni wakwao wote huwa wanakubali majukumu ya kulea watoto wao.
Kwa hiyo, issue siyo kutotumia kinga bali mtoto ni wa nani? Ndo tatizo kubwa kwa mwanaume. Kwa wale wanaojitowa akili na watoto ni wao na DNA imethibitisha kwakweli hapo sijui sababu zaidi ya kusema ''si wanaume wote are good fathers''.