SI KWELI Fatma Karume asema CHADEMA wanahusika na mauaji yanayoendelea nchini

SI KWELI Fatma Karume asema CHADEMA wanahusika na mauaji yanayoendelea nchini

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Fatuma Karume asema CHADEMA wanahusika na mauaji yanayoendelea, hatuwezi kulilaumu Jeshi la Polisi kila siku wakati viongozi wa CHADEMA wenyewe wakishutumiw na wapo kimya!

1725865814763.png
 
Tunachokijua
Fatma Karume ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, mwanaharakati ambaye aliwahi kuwa rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019. Alipata wadhifa huo baada ya kushinda katika uchaguzi wa uraisi wa chama hicho uliofanyika Aprili 2018.

Mnamo Septemba 6 2024 Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika aliandika kupitia ukurasa wake wa X kuwa "Nimetaarifiwa usiku huu kuwa Mzee Ali Mohamed Kibao Mtaalamu katika Sekretariati CHADEMA, amechukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi(bila uniforms). Walizuia basi la Tashrif alilokuwa amependa kutoka Dar es Salaam kwenda Tanga kwa gari za kawaida wakaingia na kumfunga pingu.

Tunaendelea kufuatilia kupata taarifa kamili ikiwemo wamempeleka wapi. Nimetoa taarifa hii ya awali ili iwapo kuna yoyote alikuwepo kwenye basi au ana taarifa zozote kuhusu alipopelekwa atupatie au kutupa ushirikiano wa haraka. Ambapo pia tarehe 07 Septemba 2024 Mnyika aliongea na waandishi wa habari kutoa taarifa hiyo.

Mnamo Septemba 8, 2024, Boniface Jacob alichapisha taarifa kwenye mtandao wa X akieleza kuwa Ali Mohamed Kibao amekutwa Mochwari akiwa ameuawa.

Baada ya kusambaa taarifa ya kifo cha Ali Mohamed Kibao, ilizuka taarifa iliyokuwa kwenye mfumo wa chapisho la Mtandao wa X lililotumia jina Fatuma Karume lililoandika:

"CHADEMA wanahusika na mauaji yanayoendelea, hatuwezi kulilaumu Jeshi la Polisi kila siku wakati viongozi wa CHADEMA wenyewe wakishutumiwa na wapo kimya" Tazama (hapa)

Je, Ukweli ni upi?
JamiiCheck
imebaini kuwa chapisho linalodai Fatuma Karume kasema kuwa CHADEMA wanahusika na mauaji yanayoendelea si halisi kwani limehaririwa na kupachikwa maneno kutoka kwenye akaunti halisi ya Fatuma Karume kwa lengo la kupotosha. Vilevile kwenye Akunti rasmi ya Fatuma inayodaiwa kuchapisha chapisho hilo tumebini hakuna chapisho hilo.

Aidha, Septemba 8, 2024 Fatuma Karume alichapisha chapisho la kanusho kuhusu kuhusika na maneno hayo akisema chapisho hilo ni la uzushi.

1725874205949-png.3091346

hatakama siokweli CHADEMA isitufanye tuzoee kusikia hizi taarifa ichukue hatua
 
Back
Top Bottom