ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Wana jf wengine wameacha kutumia fb ila kiukweli Ni mtandao pekee ambao ni rahisi Sana kumpata rafiki wa zamani ambaye huna mawasiliano yake ya simu.mtu nilisoma naye 1999 huko na alikuwa Ni best yangu Sana yaani rafiki tulishibana tukapotezana baada ya yeye kuhama shule ilikuwa ni darasa sa latu, hivi majuzi nikasema nijaribu ku search jina lake fb nikamuona buana. nikamuomba namba akanipa huwezi amini Ana hela hatari baba yake Ni mwanajeshi mstaafu kamwachia hela nyingi na mashamba na mang'ombe huko iringa.rafiki yangu huyu ambaye kwao Yuko peke yake leo hii tumechati naye ikanibidi nimweleze Hali halisi ya maisha yangu kwamba Sina kazi Hali mbaya kaniambia anytime nikijiskia niende iringa nikamsaidie kusimamia mashamba nyumba ya kukaa ipo.hapa Sasa hivi najipanga mwezi wa tatu naenda kukamatia fursa.anyway nisiwatoe Sana nje ya maada, ishu kubwa hapa Ni facebook asante.bila fb sijui ningekuwa Nani kwenye haya maisha.