Fb inasaidia Sana kumpata mtu mliyepotezana

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Wana jf wengine wameacha kutumia fb ila kiukweli Ni mtandao pekee ambao ni rahisi Sana kumpata rafiki wa zamani ambaye huna mawasiliano yake ya simu.mtu nilisoma naye 1999 huko na alikuwa Ni best yangu Sana yaani rafiki tulishibana tukapotezana baada ya yeye kuhama shule ilikuwa ni darasa sa latu, hivi majuzi nikasema nijaribu ku search jina lake fb nikamuona buana. nikamuomba namba akanipa huwezi amini Ana hela hatari baba yake Ni mwanajeshi mstaafu kamwachia hela nyingi na mashamba na mang'ombe huko iringa.rafiki yangu huyu ambaye kwao Yuko peke yake leo hii tumechati naye ikanibidi nimweleze Hali halisi ya maisha yangu kwamba Sina kazi Hali mbaya kaniambia anytime nikijiskia niende iringa nikamsaidie kusimamia mashamba nyumba ya kukaa ipo.hapa Sasa hivi najipanga mwezi wa tatu naenda kukamatia fursa.anyway nisiwatoe Sana nje ya maada, ishu kubwa hapa Ni facebook asante.bila fb sijui ningekuwa Nani kwenye haya maisha.
 
 
Ni kweli ila kuna wengine unakutana nao halafu wanajifanya hawataki mazoea,wengine wanachukulia ule umaarufu wa fb kupitia likes nyingi na comments kwenye post zake katika uhalisia wake,kumbe hakuna lolote.
 
Ni kweli ila kuna wengine unakutana nao halafu wanajifanya hawataki mazoea,wengine wanachukulia ule umaarufu wa fb kupitia likes nyingi na comments kwenye post zake katika uhalisia wake,kumbe hakuna lolote.
Wewe umeongea point, yaaani waweza ujioneee upo nyuma sanaa km ni mtu wa kuamini kila unachokiona kulee, kumbe weng wapo nyuma yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…