FBI/SEC yavamia makao makuu ya TELEXFREE na kuzuia akaunti za benki!

President Elect

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
693
Reaction score
212
Zaidi ya watu watano wakiwemo mabosi wa TelexFree wanashikiliwa na FBI/SEC kwa makosa ya jinai ya wizi kwa njia ya mtandao! Mamilioni ya 'wawekezaji' wanaidai TelexFree zaidi ya US$1b akiwemo mmoja toka jijini Boston aliyetumbukiza dola milioni moja na laki tatu cash.

Watu wengi pia toka barani Africa hasa katika nchi za Rwanda, Uganda, South Africa na Tanzania ni miongoni mwa wahanga wa biashara hii haramu ya upatu ya TelexFree!

source: http://www.bostonglobe.com/business/2014/04/16/feds-raid-telexfree-offices-widening-internet-fraud-probe/f1y9i2vmqNvdEtZCkcygOM/story.html
 
Me hata sijui kwa nini wajinga hawaishi duniani..
 
CC: JOYCE KORIA alidiriki kuniandikia inbox kwenye fb ila sikushawishika kujiunga!
Mungu alininusuru na hao matapeli
 
Nawashauri wahanga wa TelexFree walioko nchini Tanzania waungane na wale walioko Rwanda na Uganda wafungue kesi mahakama ya kimataifa, huenda wakaambulia chochote katika hizo raslimali zinazoshikiliwa na FBI/SEC huko Boston, U.S.A!
 
Hao si wajinga mkuu bali ni "RISK TAKERS!"

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Risk Takers Au Kuendekeza Upumbavu. We ushaambiwa its a scam na iko under investigation in the federal court of US and it was proven its a scam. Mtu kesha ambiwa yote hayo from reputable sources like www.businessforhome.org but still unakuta mtu ana peleka hela zake alizopata kwa kufanya kazi kwa bidii huko. What kind of Risk Taking is that if not STUPIDITY at its best. They have swindled millions of dollars from people. They knew what they were doing. Kitu kimefungiwa at their home country...walivyoona wataumbuka wakaja Africa to recruit new members to keep the pyramid scam going. Kama wewe ni mjanja utakua ulishasoma huo mchezo siku nyingi. Sio kila mtu ni mjinga ujue. Nilishaonya watu sana huku JF nikawaambia kuna siku wananchi watakuja mwaga kilio humu JF with this TelexFree thing, watu kama kawaida yao wakaponda sana. Na unabii wangu kweli umetimia. Risk Takers ?? Unashangaza mkuu !!! #Hahahaha
Network Marketing is a legit industry na legit network marketing opportunities zipo ndio lakini sio ujinga wa kama hawa Telexfree. Selling a product/service at overpriced prices where as u can get the same product/service for less than a dollar or free sounds extremely ridiculous to me.
 
Daaanh mie mvuja jasho niliambiwa hii taarifa nikawaambia kama kweli hao jamaa wanakupa mpunga simple hivyo katika ugumu huu mimi naona shida mbele wakanicheka sana ofisini!!!!
 
Duniani wajinga hawaishi jamani, hakuna utajiri wa bure bure namna hiyo.
 
Duniani wajinga hawaishi jamani, hakuna utajiri wa bure bure namna hiyo.

Network Marketing is truly a legit industry na kuna kampuni nyingi za halali zilizokuwa verified. Its often a mis-understood industry (wengi hawaijui na hawajui haswa inavyofanyika) Lakini kuna viji kampuni vya kishenzi vinavyo funguliwa kila baada ya dakika 5 ulimwenguni na kuwa promoted kwenye internet ndio vinachafua jina la hii industry. There is a parameter formular huwa naitumia kutambua kampuni halali na ipi ni ya magumashi/utapeli na hiyo formular haijawahi nipa majibu ya uongo hata siku moja. Nimekua nikipekua google mara kwa mara nikaipata kutoka kwa network marketing experts flan wanaotengeneza pesa ndefu sanaa kwenye hii game ya network marketing katika kuchat na kuongea nao waka share some valuable information with me. Anayetaka kujua atanijuza nimpatie. Mimi ni mjasiriamali katika mambo mengi..ila nimetokea kuvutiwa sanaa na huu mfumo wa network marketing so nimetokea kutenga muda wangu wa ziada kutaka kujua zaidi kuhusu huu mfumo wa biashara ulivyo na unavyofanya kazi, kama mjuavyo elimu ni bahari na sio siri kuna mengi sana nimejifunza.
 

Nshaongea na kuandika sana humu JF. Kwa wahanga wa hili janga sina jipya zaidi ya kuwapa pole tu. Nimesoma kwenye net leo kuna mmarekani mmoja aliwekeza $ 1 million na ushee kwenye huu mchezo wa telexfree akitarajia kutengeneza pesa nyingi...lakini aliambulia patupu na hela zote zilikwenda na maji. Mwili mzima ulitetemeka niki imagine kama ni hela zangu vile...wanasahau ya kwamba hii biashara haifanywi na mtaji mkubwa wa mamilioni ya dollar/shilingi. Hii ni biashara pekee unayoweza anza na mtaji mdogo sanaa sometimes bila hata pesa yeyote na unaweza ikuza ikawa kubwa into a million dollar business. Its all about networking with people. Bhaaas !! Nashangaa wale wanaoenda kukopa bank na ku invest mahela kibao kufanya this business. Haifanywi hivyo wakuu. Utaumia na utakula hasara bure tu. This business won't make u rich overnight. Its a process !!
What comes easy won't last, What lasts won't come easy !!
Ukishaelewa hiyo concept maishani mwako wala hupati shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…