FC Barcelona ndiye mbabe wa muda wote Spain

Mitsubish

Member
Joined
Apr 26, 2018
Posts
85
Reaction score
58
Imedhihirika jana baada ya mechi kali ya el clasico kwa mpambano ule ambao ulishuhudia Barcelona wakitumia zaidi ya dakika 50 wakicheza wakiwa pungufu ya mtu mmoja na bado wakafunga bao na wakaendelea kushambulia timu pinzani kana kwamba hakukua na upungufu.

Ikumbukwe mechi ya mzunguko wa kwanza Barcelona walishinda 3-0 uwanja wa nyumbani wa Real Madrid na oka imeanza ligi msimu huu Barcelona haijapoteza hata mchezo mmoja na imebakiza mechi tatu imalize msimu.

Hebu tuendelee kuwafuatilia Jumatano hii usiku game ya mwanzo ikifuatiwa na game ya Real Madrid na Sevilla.Hakika Barcelona ni wafalme wa muda wote La liga.
 
Nikuchokoze mkuu!?
Eti, Barca & Madrid wamekutana mara ngapi?
Aliyemfunga mwenziye mara nyingi ni nani, na kamfunga mara ngapi?
Ni nani anayeongoza kulibeba kombe la La Liga, na amelibeba mara ngapi?
Majibu yako nayahitaji sana mkuu.
 
Mkuu, Unamwita Barca mfalme!
Mfalme kwa maana ipi hasa?
Kwa kutwaa la liga mfululizo miaka ya karibuni, au kwa kutwaa Copa Del Ray, au kwa kutwaa Eufa?
Labda mimi sifahamu chochote kwenye La Liga, Naomba udadavuzi hapo, Dadavua mkuu! TUJENGANE MKUU!
 
Kitendo cha timu kumaliza mchezo ikiwa pungufu ni cha kawaida ktk soccer wala kisitumike kama porojo kisiasa au Defending policy. Ukifanya madhambi usiadhibiwe na uchekewe?
Kwani wewe ni nani usiadhibiwe?
 
Mara ngapi ktk EL Classico Madrid kamaliza akiwa pungufu?
SIMBA pungufu wameifunga Yanga mara ngapi?
Cameroun haikupigwa red card 2 mwaka 2000, Je hiyo ilimzuia kuichapa Spain na kutwaa Olimpiki?
Nigeria hakutwaa Olimpiki akiwa pungufu mwaka 1996 dhidi ya Argentina?
Ukifanya madhambi, unaadhibiwa au unakula umeme tu!
IPENDE TIMU YAKO, ILA USITIE POROJO NA SIASA KTK SOCCER.
 
Nikuchokoze mkuu!?
Eti, Barca & Madrid wamekutana mara ngapi?
Aliyemfunga mwenziye mara nyingi ni nani, na kamfunga mara ngapi?
Ni nani anayeongoza kulibeba kombe la La Liga, na amelibeba mara ngapi?
Majibu yako nayahitaji sana mkuu.
BARCA KAMFUNGA MADRID MARA 110 MADRID KAMFUNGA BARCA MARA 97
 
Cameroun haikupigwa red card 2 mwaka 2000, Je hiyo ilimzuia kuichapa Spain na kutwaa Olimpiki?
Nigeria hakutwaa Olimpiki akiwa pungufu mwaka 1996 dhidi ya Argentina?
Sidhani kama hili lipo kwenye uzi
 
Sidhani kama hili lipo kwenye uzi
Soma vizuri, kuanzia kwa mtoa uzi mpaka ktk comments za wadau utaelewa tu.
Mtoa uzi hakusema walikuwa pungufu?
Sijatoa mfano wa wale waliowahi kushinda wakiwa pungufu? AU MAHABA NIUE MKUU!?
 
Watu wengi hawaongelei uhalisia wa soccer bali ushabiki na porojo za kisiasa siasa tu, Wengine wanashabikia timu inapofanya vizuri tu, Timu ikiyumba wao wanahama. Ni wachache na makini wanaolifuatilia soccer la Spain kwa muda wote, Lakini wengine ni mahaba niue tu, Watu wengi wameikariri EPL tu, Ligi zingine hawazifuatilii bali wanampenda yule anayetwaa ubingwa tu.
 
Real Madrid ndiye Mbabe wa Ulaya
Si mbabe wa ulaya tu, Pia La Liga tangu imeanzishwa miaka yote mpaka Leo yeye ndo kinara wa kombe hilo, Halafu ktk mabingwa 10 wa vilabu wa spain wa miaka yote, Real Madrid wanashika No 1 wakifuatiwa na Athletic Bilbao, Huku Barca akishika no 3.
 
Kijana kila ligi inawababe wake. Ukitua Spain unakutana na REAL MADRID 30+ ubingwa La liga , Ukitua Italy unakutana na JUVENTUS TURIN 30+ ubingwa wa serie A . Hiyo miamba achana nayo kabisa ulaya. Sasa hivi tunasubiri nani atakua wa kwanza kufikisha vikombe 40 vya ligi kati ya Madrid na Juve. Barcelona Isingekua Dinho kuja kuifufua hadi leo Ingekua kama Real Betis tu au bahati mbaya angeshalifuata chama la ukweli enzi hizo Real Valladolid. Maana kabla ya Dinho kuja kombe lao kubwa lilikua EUROPA LEAGUE. Sababu Dinho alifanya miujiza kuwatoa mavumbini, ndio maana tumemwita Nabii Gaucho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…