FDLR waliokamatwa na M23, kurudishwa Rwanda

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
350
Reaction score
576
Leo tarehe 1 Machi, baadhi ya wapiganaji wa FDLR waliokamatwa na M23, katika vita vya Goma, vilivyoiacha Goma mikononi mwa M23, tarehe 27 January 2025, watafikishwa mpaka wa La Corniche kati ya DRC na RWanda, kukabidhiwa serikali ya Rwanda.

Baada ya kupokelewa na serikali ya Rwanda, watu hawa hupelekwa kituo cha kufunzwa uzalendo,ukizingatia waliozaliwa huko, hawana historia ya Rwanda, hufundishwa fani mbali mbali na kupewa kianzio kama mtaji. Waliohusika na mauaji dhidi ya watutsi mwaka 1994, wenyewe hupelekwa kutumikia vifungo vyao, kwa sababu wengi wao wanakuwa wamehukumiwa kipindi hawapo.

 
Kwenye mahakama za kangaroo ambako hakuna mtusi amewahi shtakiwa, wakati watutsi ndiyo walioanzisha mauaji kwa kuangusha ndege ya rais na kuwaua wahutu wengi
 
Sioni Tofauti ya Rwanda na Israel mpaka sasa
 

Live mubashara
VIDEO: M23 yakabidhi wanajeshi 14 wa FDLR kwa Rwanda akiwemo Brig. Gen Gakwerere Ezechiel na Major. Ndayambaje Gilbert Ninaomba

View: https://m.youtube.com/watch?v=rlMH85PGEyQ
'Jenerali' Gakwerere Ezechiel kiongozi mwandamizi wa wanamgambo wa FDLR na mgambo wengine 13 wamekabidhiwa kwa serikali ya Rwanda katika mpaka wa Rubavu one border stop baada ya kukamatwa nchini DR Congo na majeshi ya M23.

'Jenerali' Gakwerere Ezechiel na mgambo wenziwe wa FDLR walikamatwa ndani ya DR Congo kufuatia mapigano makali kati ya M23 na majeshi ya serikali ya FARDC yanayoshirikiana na FDLR na vikundi vingine lukuki vya mgambovikuvyojipachika jina 'wazalendo'.

FDLR ni kundi la mgambo lililokimbia kutoka Rwanda kufuatia kushindwa kampeni yao ya mauaji ya kimbari mwaka 1994 nchini Rwanda, na kukimbilia Congo kisha kutumika kuishambulia Rwanda kwa kuvuka mpaka mara kwa mara hivyo kuikera Rwanda mara kwa mara kwa mashambulizi ya kuvuka mpaka chini ya usaidizi wa,Serikali ya Kinshasa.

Picha maktaba ya Gakwerere


Picha : 'Jenerali' Gakwerere Ezechiel akiwa kituo cha mpakani cha Rubavu border post leo March 1, 2025

TOKA MAKTABA :

MAJESHI YA KIDEMOKRASIA YA UKOMBOZI WA RWANDA (FDLR)

Viongozi kadhaa waandamizi wa mgambo wa FDLR wengi wao wamewekwa katika rejista ya vikwazo, kutokana na ushiriki wao wa kuandikisha watoto jeshini kwa lazima, ukatili, utekaji na uporaji .



FDLR ni kundi la wanamgambo wenye kabila la Wahutu wenye silaha wanaofanya kazi nchini DRC. Mnamo Januari 3, 2013, OFAC iliidhinisha FDLR na M23 kwa mujibu wa Agizo la Utendaji (EO) 13413 kwa kufanya uhalifu mkubwa unaohusisha kulenga watoto katika vita vya DRC, ikiwa ni pamoja na kuandikishwa kwa jeshi pamoja na kuua, kulemaza na unyanyasaji wa kingono. M23 pia iliteuliwa kwa ajili ya kupokea silaha na nyenzo zinazohusiana na shughuli za kijeshi ambazo zilichangia moja kwa moja kwenye vita wakati huo.

Apollinaire Hakizimana (Hakizimana), raia wa Rwanda, ni kamishna wa ulinzi wa FDLR.

Brigedia Jenerali Sebastian Uwimbabazi (Uwimbabazi), raia wa Rwanda, ni kiongozi wa FDLR anayehusika na ujasusi.

Ruvugayimikore Protogene (Protogene), raia wa Rwanda, anaongoza kundi la Maccabe linaloshirikiana na FDLR, zamani lilijulikana kama Commando de Recherche et D'Action en Profondeur (CRAP). Protogene ameshutumiwa na Umoja wa Ulaya kwa kupanga, kuelekeza, au kufanya vitendo vinavyojumuisha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchini DRC, na kuwajibika kuendeleza migogoro ya silaha, ukosefu wa utulivu na usalama nchini DRC.

Hakizimana, Uwimbabazi, na Protegene zimeteuliwa kwa mujibu wa EO 13413, kama ilivyorekebishwa na EO 13671, kwa kuwa viongozi wa FDLR, taasisi ambayo mali na maslahi yao katika mali yamezuiwa kwa mujibu wa EO 13413, kama ilivyorekebishwa.

ATHARI ZA KUTIWA KATIKA REJISTA YA WAHALIFU WALIOWEKEWA VIKWAZO

Kama matokeo ya hatua ya leo, mali na maslahi yote katika mali ya watu walioteuliwa kama ilivyoelezwa hapo juu walio nchini Marekani au katika milki au udhibiti wa watu wa Marekani yamezuiwa na lazima iripotiwe kwa OFAC.

Kwa kuongezea, mali zozote zinazomilikiwa, moja kwa moja au zisizo za moja kwa moja, kibinafsi au kwa jumla, asilimia 50 au zaidi na mtu mmoja au zaidi waliozuiwa pia zimezuiwa. Isipokuwa ikiwa imeidhinishwa na leseni ya jumla au mahususi iliyotolewa na OFAC, au bila ruhusa, kanuni za OFAC kwa ujumla zinakataza shughuli zote za watu wa Marekani au ndani ya (au zinazopitia) Marekani ambazo zinahusisha mali au maslahi yoyote katika mali ya watu walioteuliwa au waliozuiwa vinginevyo.

Zaidi ya hayo, taasisi za fedha na watu wengine wanaojihusisha katika miamala au shughuli fulani na mashirika na watu binafsi walioidhinishwa wanaweza kukabiliwa na vikwazo au kukabiliwa na hatua ya utekelezaji. Makatazo hayo yanajumuisha kutoa mchango wowote au utoaji wa fedha, bidhaa, au huduma na, kwa, au kwa manufaa ya mtu yeyote aliyeteuliwa, au kupokea mchango wowote au utoaji wa fedha, bidhaa, au huduma kutoka kwa mtu yeyote kama huyo.

Nguvu na uadilifu wa vikwazo vya OFAC hautokani tu na uwezo wa OFAC wa kuteua na kuongeza watu kwenye Orodha ya SDN, lakini pia kutokana na nia yake ya kuwaondoa watu kwenye Orodha ya SDN kwa mujibu wa sheria. Lengo kuu la vikwazo sio kuadhibu, lakini kuleta mabadiliko chanya katika tabia.
Source : OFAC
 
Huyo general Gakwerere ndio muuaji wa the last Queen of Rwanda mwaka wa 1994.
 

Attachments

  • maxresdefault.jpg
    94.3 KB · Views: 1
  • 20250301_132804.jpg
    116.1 KB · Views: 2
  • 20250301_192726.jpg
    146.3 KB · Views: 2
  • 20250301_152529.jpg
    290.8 KB · Views: 2
  • 20250301_192542.jpg
    148.1 KB · Views: 2
Rwanda Rwandaaaaaa wataijua tu!!🤣🤣🤣🤣🤣
 

Attachments

  • 20250301_192731.jpg
    84.4 KB · Views: 1
  • 20250301_192726.jpg
    146.3 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…