Fedha alizompa akalipie kiwanja hajui alikozipeleka……………….!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Hebu chukulia kwamba umeoa au kuolewa na umeishi na mkeo au mumeo huyo kwa miaka nane, na mna watoto wawili katika ndoa yenu. Inatokea mnakubaliana mnunue kiwanja kutokana na kuchoshwa na nyumba za kupanga, hivyo mnaweka lengo la pamoja kuwa mtafute fedha kwa ajili ya kutimiza lengo lenu.

Inatokea kazini kwenu inajitokeza Benki moja inaingia makubaliano na kampuni yenu kwa ajili a kutoa mikopo ya muda mrefu yaani mikopo ya miaka mpaka miwili, na unaamua kukopa kiasi cha Milioni tatu baada ya kushauriana na mwenzio.Baada ya kupata fedha hizo mnatafuta Kiwanja na hatimaye mnakipata, na mnakubaliana kukilipia siku inayofuata kwa sababu mlikuwa hamtembei na hizo fedha.

Mnaporudi nyumbani unamkabidhi mwenzio hizo fedha akalipie hicho kiwanja kwa sababu wewe utakuwa bize kazini.
Baadaye unakuja kugundua kuwa mwenzio hakulipia kile kiwanja kama mlivyokubaliana na hujui fedha kazipeleka wapi……….unapomdadisi anakujibu kwa kugomba, 'bwanae usinibabaishe na vijihela vyako, nitakutafutia na kukurudishia. Wewe ulinipa nikalipie kiwanja, sasa ni kiherehere gani kilikupeleka huko kwenda kuuliza, ina maana hatuaminiani siku hizi?

Hebu niambie kama ni wewe utafanya nini?
 
Nampeleka kwanza hospitali kuthibitisha kama yuko timamu.
 
Nitamtaarifu mshenga wetu na wazazi wake wajaribu kuongea naye,mie nitatafuta safari hata ya wiki niwapishe watu hao waongee naye kwanza then nikirudi na nikapewa majibu yake nitajua nianzie wapi!
 
Kama ni mimi, ningetulia kwanza kwa muda maana ni vigumu kuamini kuwa mke wangu anaweza kuwa tapeli...... kisha ningekwenda kwa wazazi wake kujadili jambo hilo, halafu nitawaachia kazi ya kumuuliza mtoto wao alikozipeleka hizo fedha na kama nisipopata majibu ya maana........kitakachofuata ni kutalikiana na kisha kudai fedha zangu ambazo kiuhalisia si zangu bali ni za mkopo na zinatakiwa zirejeshwe na riba juu..............
 
chukua fimbo za mpera halafu unazilaza kwenye maji ya pilipili usiku mzima....
 
mmh! cjui ata ntamfanyaje hebu kwanza linikute mbona sielewi
 
mi kwa kweli nitahama nyumba kidogo ili kuweza kuweka akili yangu sawa ila nikirudi nitakuwa nahitaji majibu ya kueleweka
 
halafu hela yenyewe yamkopo ............sielewi hata nitamfanya nini........usipokuwa na kifua cha uvumilivu unaweza kumRIP
 
ngumi mbili za fastafasta...then namtwisha ndosi...inafuata kifuti....halafu namalizia na mtama....then namwinua na kumpa pole( nampaenda sana) ...namwambia kayataka yeye...!!!!!!....mmmhhh m 3 ni nyingi sana!!!!
 
"'bwanae usinibabaishe na vijihela vyako, nitakutafutia na kukurudishia. Wewe ulinipa nikalipie kiwanja, sasa ni kiherehere gani kilikupeleka huko kwenda kuuliza, ina maana hatuaminiani siku hizi?"
1. ana dharau ,
2. si mwaminifu mbele ya fedha,
3. mbinafsi anajifikiria yeye na mambo yake,
4. hajali kwa lolote wala hajutii kosa,
5. anakusingizia kosa, "......kiherehere gani kilikupeleka huko kwenda kuuliza............

maana yake;
  • Hafai katika majukumu ya maendeleo ya familia
  • fikiria njia mbadala ya kufanikisha mambo yako
 

Umenifurahisha sana na maoni yako.............................
 
duh! hizi ndoa ni mtihani.niliwahi kukutana na kaka mmoja wa togo,akanipa stori yake nilimhurumia sana. yeye anafanya kazi nje ya nchi,mke anamuibia hela hadi za kwenye account kwa kufoji documents!jamaa akiacha hela ya matumizi mamaa anachakachua yote. akinunua mabati,nondo,mchele na sukari wife anaenda kuuza bei rahisi dukani! nikamuambia kama ni mtihani wa hivyo mi nafeli straight away,nachoma daftari na nikishawishika najikata mkono! kazi kweli kweli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…