SoC02 "Fedha iliyopo msituni" kauli ya baba

SoC02 "Fedha iliyopo msituni" kauli ya baba

Stories of Change - 2022 Competition

Sakho

Member
Joined
Sep 5, 2022
Posts
6
Reaction score
5
Nisingeweza kufika hatua ya kuandika ndan ya jukwaa la jamii forums bila Mali ambazo zimepatikana msituni.

Mimi ni mwanafunzi mwenye elimu ya chuo kikuu, mafanikio yangu yametokana na bidii ya baba yangu kupanda miti miaka ya nyuma sana ambayo imesaidia katika kunisomesha mimi na ndugu zangu.

Misitu ni raslimali muhimu katika taifa letu na inatakiwa kutunzwa kutokana na umuhimu mkubwa tunaoupata kutoka kwenye raslimali hii, Kuna misitu ya aina mbili ambayo ni misitu ya asili na misitu ya kupanda.

Ukweli juu ya kauli ya fedha ipo msituni na umuhimu wake
Mnamo mwaka 2019 nilifanikiwa kupata nafasi ya kwenda kusoma chuo Sokoine university of Agriculture, Bachelor of science in Biotechnology and Laboratory Science lakini furaha yangu ilizimwa baada ya kukosa mkopo ambao ungenisaidia pindi nasoma chuoni, kwani wazazi wangu ni maskini hivyo wasingeweza kumudu gharama za kunisomesha huko.. skuwa na Raha kwa sababu ndoto zangu ilikuwa ni kusoma na kufika elimu ya chuo kikuu.

Hii ilimuumiza sana kichwa baba yangu niliyekuwa nikimtegemea kwan alinisomesha kutoka chekechea mpaka form six kwa wakati huo lakini Mungu si Athumani baba yangu alikuwa na shamab kubwa la miti aina ya pines aliyopanda miaka ya nyuma kidogo, na kwa kuwa alikuwa kiongozi wa kanisa la nyumbani, kulikuwa na uanzishwaji wa makao makuu ya parokia (mission) na walikuwa wakihitaji mbao nyingi kwa ajili ya ujenzi baba yangu hakusita kuwaambia kuhusu kuuza miti hiyo na ukizingatia alikuwa na uhitaji. Ili aweze kunipeleka shule, walikubali ombi lake na kununua miti ile na hatimaye niliweza kwenda chuoni kuendelea na masomo..kwa hiyo wananchii hawana budi kupanda miti kwa bidii Ili kiabiliana na changamoto za kiuchumi na kuweza kumudu gharama za maisha ya kila sku . " MISITU NI MALI".

Uhalisia
Kwa kawaida kwa miti yenye miaka kumi, mti mmoja unauzwa 10000 kwa hiyo ukiwa na miti 500, unauza na kupata SI chini ya millioni tano. Hii ndo maana halisi ya fedha iko msituni japo inahtaji kupanda mapema na kutunza kwa ajili ya matumizi ya baadae.

UMUHIMU MWINGINE
#Misitu au upandaji wa miti unatusaidia kuepuka ukame,
Kwa sababu misitu au miti ni muhimu katika kutengeneza mzunguko wa maji ( water cycle)ambayo husaidia upatikanaji wa mvua muda mwingi katika eneo husika.

# Upatikanaji wa hewa safi (Oxygen)
Mimea hutumia hewa chafu itolewayo na wanyama katika kusanisi chakula chake na kutengeneza nishati, hewa hiyo huitwa kabondayokisaidi lakini mimea hutoa oxygen inayotumika kama hewa safi kwa wanyama, mbadilishano huu wa gesi husaidia kupunguza kiwango cha hewa chafu kwenye mazingira mfano angani, ambayo pia inasaidia kupunguza uchafuzi wa anga na kuharibika kwa tabaka la ozoni( ozone layer).

# Hutumika kama makazi ya viumbe mbalimbali
Wanyama na wadudu mbalimbali wanategemea misitu Ili waweze kuishi hii ndo maana halisi ya kutegemea na muingiliano baina ya viumbe hao.

#Utoaji wa nishati mbalimbali mfano Kuni na mkaa ambazo asilimia kubwa ya watanzia hutumia majumbani mwao kwa shughuli mbalimbali
 
Upvote 4
Back
Top Bottom