Fedha za DHAMANA

ukisikia ukwasi ndio huo sasa!!!! mali za bilioni sio tatizo. mbaya zaidi watu wa madini hao hao kina senkoro wamekuja kutoa dhamana!!!interesting
 



Kwenye bold; Hapo ndipo tatizo lilipo. Haya mengine yoote, tunapoteza muda. Mimi sio mchumi/mhasibu wala mtaalamu wa Finance ila nadhani dhamani ya nyumba/ kiwanja Tanzania wanapima kwa kuangalia potential "demand" yake.

Sasa naomba wenye utaalamu wa haya mambo ya valuation watusadie; nisije nikawa naendelea kubeba mabox huku ughaibuni kumbe nina dola milioni kadhaa kwenye viamba vyangu pale jijini. Msaada tafadhali hii suala ni nyeti.
 
Anglo Ashanti yakwao pia..angalia picha za kutoka mahakamani utaona CEO wa anglo ashanti anashuka nao ngazi...watu wanahela hawa ogopa!!
 

Du huyu mzee poa sana! mungu ambariki
 

Wakubwa mkumbuke tu kuwa mapato ya mtu si mshahara peke yake. Mie pia ni mfanyakazi wa serikali lakini nina miradi yangu inanipatia kila mwezi zaidi ya mara 3 ya mshahara wa serikali ninaopata. Ninafuga nguruwe na kuku, tuna mgahawa (niwe mkweli tu, 'mama ntilie'), genge la mbogamboga, baa (inayosapotiwa sana na kitimoto ninaofuga), na tangu mwanangu mkubwa amalize chuo amekuwa akiniunga mkono kwenye biashara ya internet cafe na mambo ya secretarial tuliyomwanzishia apate ajira. Sasa hapo ukinikadiria mapato yangu kwa kutumia mshahara wangu wa serikalini utakuwa unanishusha sana. Siwatetei hao jamaa kwa kuwa na hela hizo, lakini kabla ya kuhukumu kama ni za halali au la, tuangalie kwanza vyanzo vyao vyote vya mapato na kiasi kinachozalishwa humo.
 

Mkuu Mwikimbi wewe ni mtu wa karibu kwenye zoezi la dhamana za BOT. Nina maswali machache
1. Je wafungwa wote magerezani wamehukumiwa na Mhe. Hakimu Mwankenja? Kwani watuhumiwa wakipatikana na kosa, kuhukumiwa ni kosa?
2. Kama ni hakimu asiyefuata sheria, kuna taarifa za hukumu za hisia? Please hapa ni JF where we dare to talk openly ziweke hapa
 

Mzee, Hakimu Mwankenja ni mmoja kati ya mahakimu wachache sana tulionao ambao wanafanya kazi kwa uadilifu na MAADILI ya hali ya juu sana. Ni mchungu sana kwa wabadhirifu, wezi, ...,. Badala ya kumponda kwa kuwa tu ndugu, jamaa, rafiki kanyimwa dhamana tuangalie na tutangulize maslahi ya nchi kwanza.
 

I agree with you. Kitendo cha hukumu/maamuzi fulani kutenguliwa na mahaka ya juu yake haimaanishi moja kwa moja kuna udhaifu ktk hukumu ya awali. Ndio maana kumekuwa na hierarchy ktk mahakama (Primary court, Resident Magistrate Court, High Court, Appeals Court etc). Inawezekana kabisa kama upande wa mashtaka ungekata rufaa, tungeona maamuzi ya mahakama ya rufaa reinstate maamuzi ya Mwankenja!

Kwa Tanzania jinsi ilivyo, siwezi kushangaa kwamba kuna mlungula ulitembea ktk mahakama ya juu ili kuwasaidia vigogo hawa. Masha alienda kufanya nini gerezani? any connection? Na hisi kuna mambo bado yamejificha ambayo watu wa kawaida kama mimi na wewe hatuwezi kuyaona.
 

Huu mjadala unafurahisha sana.
Wakuu wote mliokasirishwa na utendaji wa Hakimu Mwankenja nafikiri mna haki kujisikia vingine kwa maana katika shauri hili kuna pande mbili.Wanaowaonea huruma watuhumiwa na wasioona huruma kwa watuhumiwa. Kwa wale wasiofungamana na upande wowote nadhani mjadala huu unaweza usiwe na maana kubwa sana .Kufuatana na uzoefu na uelewa wangu katika utendaji wa kisheria ikiwemo mahakama, nadhani si vema kumhukumu hakimu huyu moja kwa moja bila kuangalia nini hasa hutokea kabla ya uamuzi wa mahakama kutolewa.
Kuna vitu vingi sana vinavyochangia kuathiri utoaji wa hukumu au amri mbalimbali. Kuna sheria, taratibu, kanuni na hata public policy ( which has been said to be an unrully horse and hence difficult to define).Tusisahau kuwa hakimu au jaji ni mwanajamii pia hivyo itakuwa uongo kusema ati haathiriwa au kushawishiwa na mtizamo wa jamii alimo.

Tukumbuke pia kwamba haya mashauri ya mafisadi hayakuzuka tu kama mashauri mengine tuliyozoea kuyaona au kuyasikia kila siku.Haya ni mashauri yaliyotokana na kilio cha umma wa Watanzania.Hivyo itakuwa ajabu kwa mahakama kufanya "business as usual" na kuchukulia kijuujuu tu kama vile si kitu kikubwa.Vilevile kuna landmark cases ambazo mwisho wake wale walioshiriki kuzishughulikia kwa namna moja ama nyingine wanaacha a mark in building of jurisprudence.Hapa ndipo utaona maamuzi bold kama haya ya akina Mwankenja na katika fani nafasi hizi ni finyu na adimu!Tayari Mwankenja kwa mfano ameshaingia katika kumbukumbu si za historia ya Tanzania tu bali hata kumbukumbu za kisheria kwa msimamo wake, uwe mzuri au mbaya.

Kama walivyochangia wengine hapo juu, kisheria hakimu alitoa maamuzi yake ndani ya taratibu zinazokubalika na kufuatana na uwezo aliopewa kisheria.Kilichofanyika mahakama kuu ni utaratibu wa kawaida wa kusikiliza rufaa kulingana na sababu zilizotolewa na kutoa uamuzi.Ni kitu cha kawaida kabisa na siyo ati kwa vile Mwankenja alikosea au kukiuka utaratibu wowote.

Hayo mengine kwamba Mwankenja alitaka kubadili msimamo wake na kulegeza masharti nashindwa kuyakubali maana kisheria Hakimuau Jaji akishatoa uamuzi wake basi unamfunga na hawezi kuubadilisha yeye labda ukabadilishwe ngazi ya juu yake ( anakuwa functus officio na hii ni kanuni kuu katika utendaji haki vinginevyo basi kusingekuwa na kutabirika katika utoaji hukumu au amri maana ingekuwa na ukigeugeu na abuse of power/authority kusiko na kikomo.
Baada ya ufafanuzi huu mfupi ni juu yetu sasa kuamua kama kilichotendeka ni sawa au la katika misingi ya sheria bila kuweka jazba.
 
Huwa wanaweka bond yenye thamani sawa ana kiasi cha fedha zilizotajwa na si fenda taslim, nadhani Kina Mramba waliamua kuwakomoa ndio wakataka cash.

Ingawa bado najiuliza,, kwa watumishi waumma hawa inawekanaje wamiliki mali yenye thamani kubwa hivi?
 

Mkuu sidhani kama kuna mtu anasema kuwa mapato yako yote yatokane na mshahara tu. Ila tunategemea kuwa mapato yako mengine nje ya mshahara yatatokana na shughuli halali. Kwa hiyo hutakuwa na taabu ya kuthibitisha chanzo cha utajiri wako. Utashusha tu TAX RETURNS zako na kila mtu ataridhika. Ila kama hutaweza kutushawishi kwa kutuonesha uthibitisho basi hatutalaumiwa kukuita fisadi, na Keko itakuwa ndo mahali panapokufaa.

Kwa Tz nadhani ni rahisi sana kukamata mafisadi kwa sababu moja rahisi. Mwambie kila mtu akupe uthibitisho kuwa mali zake ni halali na analipia kodi. Hapo wengi wetu tutauvaa mkenge. Kama tungekuwa na serikali makini mahali pa kuanzia ni hapo tu na njia rahisi sana. Vinginevyo tutakuwa kama BWM aliyewahi kushangaa kuwa watu wanapata wapi pesa za kushusha majumba wakati njia zote amezibana. May be ndo maana na yeye akashtuka na kuanza kuchukua chake mapema.
 
Alafu na izo zamana za mahera yote hayo si ushahidi tosha wamekwiba ela zetu jamani.Ata kama wanachangiwa ni yale hao washikji alikuwa anakula nao leo wameona wasimtose mtuu wao.
Sijui lini tutaja kuwa serious oncemore kama viongozi wa nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…