VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Ni ishara na uthibitisho wa ufisadi.Ni pale Chuo Kikuu cha Dodoma almaarufu kama UDOM.Fedha kwa ajili ya mkopo wa ada kwa wanafunzi waliomaliza chuoni hapo mwaka jana zimeyeyuka.Wanafunzi hao ambao wanamiminika Chuoni hapo kwa ajili ya kuchukua 'Transcripts' na vyeti vyao wamejikuta wakidaiwa fedha kuanzia laki tatu na arobaini na kuendelea hadi milioni moja na ushee.
Kilichotokea
Taarifa zilizonifikia zinaonyesha kuwa wanafunzi hao walitakiwa kusaini(walipokuwa mwaka wa kwanza 2008) fomu maalumu toka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili kuonyesha kupokea kwao fedha walizolipiwa na Bodi.Zilitakiwa zijazwe fomu mbilimbili.Uongozi wa Chuo ukawasainisha fomu mojamoja.Tatizo kubwa.
Fedha zikaonyesha zimelipwa nusu ya kiasi kilichotakiwa.Wanafunzi walipokwenda Bodi-Tawi la Dodoma kuulizia kuhusu madeni wasiyoyatarajia,walielezwa kuwa fedha hizo zilishapelekwa UDOM na hazikuwahi kurudishwa.UDOM wakadai fedha hizo zilisharudishwa Bodi.Dana dana.Maumivu kwa wanafunzi.Wengi wa wanafunzi wameshindwa kuchukua vyeti vyao.Fedha zimeyeyuka.Nani amekula pesa hizi? Na ajitokeze...