Mkuu zingatia kwamba benki haiendeshwi kwa vyombo vya habari. Kinachozungumzwa ni umiliki wa benki na sio operations za benki. Serikali ndo inatakiwa kuumiza kichwa hapa ili kulipa deni la absa. Kama haitalipa serikali itapoteza hisa zake lakini operations zinaendelea. Ifahamike kwamba kuna viashiria kadhaa vinavyoweza kuonesha hii taasisi inakufa ama la. Kwa mfani kupata hasara, kushindwa kulipa madeni na kugharimia shughuli zake, key ratios ku-deteriorate n.k. Nbc so far sioni shida hiyo japo tunasikia non performing loans ziko juu. Ikumbukwe kwamba hizi non performing loans kuna watanzania kibao wamekopa huko na hawana utayari wa kurejesha. Kwa hiyo kama hii benki inakufa leo kuna watanzania wengi watahitaji lawama. Sio tu walioiuza kwa bei chee bali pia na wale ambao wanakopa halafu hawataki kurejesha
yaani ABSA tumewapa bank kwa bei ya kutupa na majengo kila kitu wamekuja mikono mitupu,bado na pesa tuwape tena?sasa kuna faida gani ya huyu muwekezaji?kila mkataba eerilali huishia kuingia mfukoni kumlipa muwekezajiMkuu zingatia kwamba benki haiendeshwi kwa vyombo vya habari. Kinachozungumzwa ni umiliki wa benki na sio operations za benki. Serikali ndo inatakiwa kuumiza kichwa hapa ili kulipa deni la absa. Kama haitalipa serikali itapoteza hisa zake lakini operations zinaendelea. Ifahamike kwamba kuna viashiria kadhaa vinavyoweza kuonesha hii taasisi inakufa ama la. Kwa mfani kupata hasara, kushindwa kulipa madeni na kugharimia shughuli zake, key ratios ku-deteriorate n.k. Nbc so far sioni shida hiyo japo tunasikia non performing loans ziko juu. Ikumbukwe kwamba hizi non performing loans kuna watanzania kibao wamekopa huko na hawana utayari wa kurejesha. Kwa hiyo kama hii benki inakufa leo kuna watanzania wengi watahitaji lawama. Sio tu walioiuza kwa bei chee bali pia na wale ambao wanakopa halafu hawataki kurejesha
Kuhusu uendeshaji wa mashirika ya umma na usimamizi wa rasilimali zetu ni kweli kuna tatizo kubwa. ni kwa sababu kila mtu anawaza achukue cha kwake asepe. Hata hizo sheria zinatungwa na hao hao ili zije kuwakinga wenyewe. Kuna kitu lazima kifanyike, tunaanzia wapi hilo ndo gumu. Mfumo wa maisha yetu umekaa kwa namna ambayo fikra za ukombozi hazipo tena na kila mtu anawaza ntapataje hela nile, nionekane ninazo. Ubinafsi tu umetujaa. Kulikomboa taifa hili na rasilimali zake ni lazima watu kadhaa wajisacrifice for tomorrow of Tanzania. Issue hapa ni nani atamfunga paka kengele?
Hii benki mi inanipa hofu kuliko. Hapa ninapotoa hii comment siwezi kuaccess account yangu wala kutoa hela eti siku-update taarifa zangu na itanibidi kusubiri mwezi mmoja hadi miwili taarifa zangu wazi-update ndo niwe na access na acount yangu. Jamani naomba mnisaidie kwa hili nifanyeje? Hivi ni kweli mmiliki wa account ku-update taarifa zake kuchukue muda hivyo? 1-2 months?Wana jf heshima kwenu.
Naomba kuuliza ili kuondoa hofu/au kupata uhakika na sakata linaloendelea ndani ya NBC.
Sie walala hoi tuliohifadhi vijisenti vyetu huko NBC hatupati usingizi tunaweweseka na kupata nusu wazimu.
Tulishawahi kulizwa na bank iliyokuwa inaitwa meridian biao je? haya hayawezi kutokea NBC?
Maelezo yaliyitolewa na benki kuu BOT ndio yameongeza hofu zaidi
(zingatia kila maelezo yanayotolewa na serikali pamoja na vyombo vyake hayaaminiki asilani/huzidi kutia hofu)
Kwa sisi watu masikini ni bank ipi inatufaa?
Natanguliza shukran za dhati.
Student spotted. :mmph::mmph:Thats not true...mayb uwe umekosea hizo information umeambiwa lete hiki ukapeleka kile ndipo watanzania wengi tulivyo tunapenda vitu faster faster pasipo kutulia na kufuata nini tunaagizwa kufanya ili kutekeleza hitaji letu ASAPs