Fedheha kubwa kwa wizara ya elimu.

Joined
Dec 6, 2012
Posts
7
Reaction score
0
Cha kushangaza ndugu watanzania hamuwezi kuami kwamba serikali inayoongozwa na CCM ina shule moja tu ya kufundishia wanafunzi wenye ulemavu wa kusika, iitwayo kigwe iliyoko wilaya ya bahi mkoa wa Dodoma. shule nyingine mnazozijua za walemavu zina mikono ya wafadhili wa nje na nyingi zinaongozwa na mashirika ya dini, kilichoniumiza ni pale nilipoona wanafunzi wa shule hiyo wakirudishwa nyumbani kabla ya kumalizika kwa muhula wa masomo eti kwa kukosa huduma za msingi ikiwemo chakula. wamebaki wale wa darasa la saba tu.
kama hujui ndugu nikufahamishe kwamba watoto hawa wanasoma shule ya msingi kwa miaka 10 badala ya saba (7). hii ni kutokana na uwezo wao wa kuelewa mambo taratibu, sasa kama tena shule inafungwa kabla ya wakati kweli tunawatakia mema hawa wanafunzi?
wakati wizara ya elimu inaenda kuwasilisha bajeti yake ninaomba nimuulize waziri je watu binafsi wanafedha kuliko serikali? mbona shule zao hazifungwi kabla ya wakati? isipokuwa shule hii ya watoto hawa wenyeulemavu.
au serikali ya CCM inawabagua hawa kwa kuwa ni walemavu?
waziri atujibu swali hili. na serikali atachukua hatua gani kuwasaidia watoto hawa.
 
kingine umesahau mkuu wana ndege moja tu na wafanyakazi lundo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…