je parle
JF-Expert Member
- Nov 28, 2018
- 2,022
- 3,919
Kanuni na Sheria za Mpira huwa zinawakandamiza sana wachezaji na kuinufaisha club, mara nyingi ndio huwa hivyo.
Timu inaweza kumsajili mchezaji na asipo perfome vizuri huwa zinaweza tamatisha mkataba wake na kumlipa kahela kadogo akatafuta timu nyingine na kuanza maisha mapya.
Na sote ni mashahidi wa hilo hawa Yanga ndio wanaongoza kwa kutoa wachezaji kwa kumkopo na mwisho wa siku kuwatema kwa kuwa viwango vyao hawajaridhika navyo.
Sasa iweje mchezaji akiwa katika kiwango bora na yeye akipata timu sahihi asiweze kuhama timu kwa kuipa posho timu yake ya sasa?
Kwanini timu zinaweka ngumu mchezaji anapotaka kuondoka?
Tumeona Simba wakufanya hivyo kwa wachezaji kutaka kuondoka na wao kuwapa mkono wa kwaheri vizuri tu.
Lakini Yanga wao imekuwa nongwa mchezaji akitaka kuondoka kwao ni purukushani na agenda za uchonganishi.
Tumeona kwa ajibu na Gadiel hawa vijana waliwapiga vipapai kabisa wasiwepo katika ramani ya Mpira.
Walifikia hata kuwatishia maisha kuwa huko wanapoenda hawatoboi.
Kweli ile timu fulani wenye akili ni wawili kwa mujibu wa Mr Misifa.
Yanga muacheni fei toto mara moja kwa kuwa tayar mkataba ulishasema kuwa ukitaka kuvunja mkataba unalipa signing fee na mshahara wa miezi mitatu na yote hayo fei kafanya
Sasa sijui mnataka Nini kwake zaidi ya hicho, labda roho yake.
Kama mlikuwa hamtaki aondoke hapo club kwann mliweka hicho kipengele?
FEI Fanya mazoezi yako yanga usirudi baki na msimamo huo huo usiwe kama sizitaki mbichi hizi
Watakuacha ni suala la muda tu.
Na usije ukasign Simba watakupiga ndumba hao jamaa kwa tunguri wapo vyema
Note:
Tanzania tunatakiwa kuwa na Sheria zetu za Mpira hizi za wazungu zinatuchanganya.
Tusiwaige wazungu katika Sheria tu lakini katika mikataba na Mishahara tunababaisha
Itakuwa sio vyema.