Fei Toto aachwe akatafute maisha sehemu anayoona inamfaa, Sheria za Mpira zinakandamiza sana wachezaji

je parle

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Posts
2,022
Reaction score
3,919
Kanuni na Sheria za Mpira huwa zinawakandamiza sana wachezaji na kuinufaisha club, mara nyingi ndio huwa hivyo.

Timu inaweza kumsajili mchezaji na asipo perfome vizuri huwa zinaweza tamatisha mkataba wake na kumlipa kahela kadogo akatafuta timu nyingine na kuanza maisha mapya.

Na sote ni mashahidi wa hilo hawa Yanga ndio wanaongoza kwa kutoa wachezaji kwa kumkopo na mwisho wa siku kuwatema kwa kuwa viwango vyao hawajaridhika navyo.

Sasa iweje mchezaji akiwa katika kiwango bora na yeye akipata timu sahihi asiweze kuhama timu kwa kuipa posho timu yake ya sasa?

Kwanini timu zinaweka ngumu mchezaji anapotaka kuondoka?

Tumeona Simba wakufanya hivyo kwa wachezaji kutaka kuondoka na wao kuwapa mkono wa kwaheri vizuri tu.

Lakini Yanga wao imekuwa nongwa mchezaji akitaka kuondoka kwao ni purukushani na agenda za uchonganishi.

Tumeona kwa ajibu na Gadiel hawa vijana waliwapiga vipapai kabisa wasiwepo katika ramani ya Mpira.

Walifikia hata kuwatishia maisha kuwa huko wanapoenda hawatoboi.

Kweli ile timu fulani wenye akili ni wawili kwa mujibu wa Mr Misifa.

Yanga muacheni fei toto mara moja kwa kuwa tayar mkataba ulishasema kuwa ukitaka kuvunja mkataba unalipa signing fee na mshahara wa miezi mitatu na yote hayo fei kafanya

Sasa sijui mnataka Nini kwake zaidi ya hicho, labda roho yake.

Kama mlikuwa hamtaki aondoke hapo club kwann mliweka hicho kipengele?

FEI Fanya mazoezi yako yanga usirudi baki na msimamo huo huo usiwe kama sizitaki mbichi hizi

Watakuacha ni suala la muda tu.

Na usije ukasign Simba watakupiga ndumba hao jamaa kwa tunguri wapo vyema

Note:
Tanzania tunatakiwa kuwa na Sheria zetu za Mpira hizi za wazungu zinatuchanganya.

Tusiwaige wazungu katika Sheria tu lakini katika mikataba na Mishahara tunababaisha
Itakuwa sio vyema.
 
Aendelee kuyatafutia hapohapo Yanga. Kwani kuna shida?
 
Upo sahihi mkuu ila kumbuka kuna wajibu wa kisheria, ni wajibu wa mhusika kujua hili, huwezi kuvunja mkataba wako bila kufuata mkataba umesema nini
 

🤝🤝
 
Hakuna kitu kama hicho, sheria ya mpira ipo kote kote wala hakuna anayebebwa zaidi ya mwingine. Kwasababu mkataba ni makubaliano ya pande zote mbili, mchezaji akitaka kuvunja mkataba ni lazima waafikiane na mwajiri. Na pia mwajiri akitaka kuvunja mikataba ni lazima afikiane na mchezaji.

Kuna wachezaji wanasajikiwa halafu hawaoneshi kiwango cha kuvutia lakini hapo kumvunjia mkataba ni mpaka mchezaji husika aridhie. Sheria ni msumeno hukata huku na kule.
 
Kijana wa watu muadilifu kukataa ushoga ndiyo anapata usumbufu wote huu. Upinde wabaya sana
 
Hata timu ikiona mchezaji hakidhi mahitaji hawamfukuzi ila wanakubaliana kuditisha mkataba au atolewe Kwa uhamisho na sio kutumia mkato Kama alivyofanya huyo ndugu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wewe si mfuatiliaji wa michezo hilo ndio hitimisho langu. Juzi tu hapa Simba wamehangaika saana kumtoa Okwa na Yanga kumtoa kiungo Mrundi Bigirimana na Kambole. Mkataba ni suala la kisheria sio holela holela tu.
 
Kila kitu kinafanyika kwa makubaliano. Hao Yanga hawakurupuki tu kuvunja mikataba na hao wachezaji walioshuka viwango. Wanakaa mezani, na kufikia muafaka.

Sasa uniambie huyo Fei Toto alikaa na viongozi gani wa Yanga ili kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake?
 
Kila kitu kinafanyika kwa makubaliano. Hao Yanga hawakurupuki tu kuvunja mikataba na hao wachezaji walioshuka viwango. Wanakaa mezani, na kufikia muafaka...
Kukaa na kukubaliana pia ni suala la kimkataba. Kwa nini iwe ni lazima kukaa na kukubaliana kama haipo kimkataba?
 
Wewe hujui Sheria za mpira. Si ajabu umezitoa kwenye kahawa.
 
Wachawi wa kinyesi fc,walishataka kumuua kwa ajali,ila waswahili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…