kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kijana amevurugwa kichwa, wenye hela wamemvuruga moyo, pepo la fedha nyingi za ghafla likamrukia shingoni.
Hapo alipofikia Sasa hahitaji msaada wa wanasheria bali wanamaombi ili kumtoa pepo la tamaa na choyo lililomfunika. Wanasheria watamharibia zaidi kipaji chache.
Fei Toto anahitaji watu neutral wampatie utulivu wa akili kabla ya kumuelewesha pale alipokosea na afanye nini kuokoa kilichobaki kabla ya Mei 2024.
Familia ya Fei washauriwe watafute njia nyingine za kujikimu ili Fei aende polepole kufika kule waliko akina Chama, Mbwana, Mayele, Saido, Bangala, Inonga, na akina Manula na Diara. Kuna mchakato wa kufikia hatua hizi na sio kwa kufunga magoli 3 tU kwenye mechi ngumu za timu.
Kama TFF wangeamua kwa hovyo kesi hii basi timu ndogo zote zingenyang'anywa wachezaji wao wazuri kwenda timu kubwa kiholela. Kama Yanga imenyang'anywa kwa aina hii itakuwa ruvu shooting na mlandege FC?
Ni bora TFF imeuona upuuzi huu mapema, hongera sana TFF kwa malezi haya. Kinachofuata ni adhabu Kali kwa wote walioko nyuma ya upuuzi huu unaoelekea kwenda kuua kipaji Cha mtoto anaeinukia kisoka. Walidhani wataambiwa walipe faini tu kwa kuvunja mkataba kimakosa ili kuondoka na Fei, lakini hesabu zao zimegonga ukuta. kama ingekuwa rahisi hivyo hata akina mbappe, halaand, messi, Pogba na Ronaldo wangeshasepea kwingine fasta kufuata pesa nyingi kwa matajiri
Tunajua kwamba Yanga Haina shida na kumuachia Fei aondoke zake, lakini kama watafanya hivyo watakuwa wamekosea sana Leo na hata kesho. Watashindwa kufanya vinginevyo kwa case itakayofanana na hii huko mbele.
Kila mtu mwenye ujuzi na karama ya kutuliza pepo mchafu amsaidie kijana wetu.