Fei Toto anusurika ajalini Fuoni

Fei Toto anusurika ajalini Fuoni

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mchezaji wa Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania Feisal Salum Abdallah (Fei toto) amepata ajali mchana wa leo Fuoni, Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.

Ajali hiyo imehusisha Gari yake aina ya Harrier nyeupe yenye namba za usajili Z 160 MW huku dereva akiwa ni mwenyewe Feitoto akitokea Fuoni kituo cha zamani akielekea Mjini ndipo ilipogongana na Bodaboda yenye namba za usajili Z 423 KL.

Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha wala kuumia zaidi ya Gari kuharibika mbele na Bodaboda imeharibika ambapo mpaka sasa Vyombo hivyo vipo kituo cha Polisi Fuoni.

"Ni kweli imetoka ajali hapa Fuoni Gari aina ya Harrier imegongana na Bodaboda, Gari ni ya yule bwana mdogo mchezaji wa Yanga Fei, lakini ni ajali ndogo tu hakuna aliyeumia"-Mkuu wa Kituo Cha Polisi Fuoni.
 
Shaffih Dauda ni bonge la fala yani

Nimeiona hii habari kaiandika kishambenga sana

Title ya Bandiko lake kasema "Feisal anusurika kifo"

Anafanya hivyo kwa ajili ya upumbavu wa kitoto tu kwa ajili ya ku catch attention watu wasome the whole story
 
Katoto kajinga sana hako! Wenzake wanashiriki mashindano ya ndani na pia yale ya Kimataifa! Kenyewe kako busy kushindana na timu kubwa, na ya wananchi kama Yanga!

Yaani bora kuwa na kisogo, kuliko kuwa na kichwa flat!
Ndo mumroge afe ? Ukiwa utopolo akili zako zote equal to 0
 
Back
Top Bottom