Fei Toto kama umeshindwa, sema tukusaidie

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Maswali yalikuwa mengi sana kwanini Feisal anachezeshwa kwenye double pivot, kwanini Feisal aisipelekwe namba [emoji647]? Naamini Mwananchi ulijiuliza sana

Kwanini Feisal anachezeshwa eneo la kati au chini karibu na goli? Kwanini Kocha anamweka 'eneo sio lake' kifupi Kocha hajui kumtumia Feisal, yalikuwa maneno yenu Wananchi

Labda niwaambie kwanini Feisal alikuwa anawekwa pale, kwenye mpira kuna nafasi na Majukumu, ROLES AND POSITION, Feisal alipaswa kutafsiri majukumu kwenye eneo lake

Makocha walichotaka ni kuwa build up ya timu ianzie chini, mabeki wa kati mpira waupeleke shimoni (Eneo la kiungo) hii iwape nafasi mabeki wa pembeni kuoverlapp na kutanua uwanja (width play)

Sio kwamba Feisal alishindwa kabisa kutekeleza majukumu, aliweza kwa kiasi chake ila alihitaji mtu wa kumwonesha kwa vitendo namna gani (Regista role) inafanywa, alihitaji case study

Ghafla amekuja Carlinhos, Mchezaji anaecheza basic football tukumbuke mpira halisi ni kama Draft yani One touch, yeye amewekwa eneo kama la Feisal na majukumu kama ya Feisal

Mtazame jana alipokuwa anaombea mpira, kwenye halfspaces sehemu ambazo yupo free na mtazame wapi anaswitch mpira, kwenye eneo ambalo wachezaji wapo free

Carlinhos amefaulu kwenye passing, amefaulu kwenye kutafsiri mchezo lakini pia amefaulu kwenye coverage ya uwanja, inside passes ni brilliant kabla hajagusa mpira ameshaona watu watatu mbele

Kuna muda alikuwa chini kabisa karibu na beki za kati, kuna muda alikuwa pembeni karibu na Fullbacks na kuna muda alikuwa mbele kabisa, aliutafsiri mchezo wa jana na kuufuma mchezo mzuri wa soka

Hatuwezi mlaumu Feisal kwakuwa huyu Mreno amefundishwa, sisi wetu hapa kipaji tu kinatuongoza, wenzetu wa NURTURE na NATURE kwenye talent zao, nadhani jana Feisal kaendelea kupata somo

Naomba kuwasilisha
 
Honestly, ukiachana na pass za square,chenga na kukaa na mipira bila sababu,Feisal nampa F kwenye visionary passes na kutimiza majukumu ya namba yake...F kabisa FaFaFa!
 
Duu wachambuzi wetu wa kizazi kipya jamani double pivot ndiyo kitu gani sasa tumieni kiswahili nasisi tuelewe.
 
Kila mara nasema wachezaji wetu wazawa ukiondoa angalau mabeki na kipa ambao wanajitahidi,nafasi za kati na ushambuliaji bado zero kabisa,tungesajiri wageni tu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…