Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Messi wa Bongo alikutana na kina Jemadari Said wa kipindi hicho wakamwambia Simba ni kitu gani ondoka na wakikataa watukane wakufukuze. Leo imebaki historia.Inasikitisha sana! Kiukweli nauona mwisho wa kijana huyu, kwa kweli ni majonzi.
Nakumbuka kuna kijana aliitwa Singano, na aliitwa Messi pia, lakini baada ya kupata umaarufu akalewa na akajakuwa kama Fei toto, lakini baada ya muda mfupi hajulikani alipo.
Sidhani, maana kwa Tanzania, timu za mchezaji kuweza kisimama ni Simba na yanga tu, na yanga ameshaharibu tayari,Fei atasimama tena , Mungu awe nae[emoji28][emoji28]
Iende sambamba na uboreshwaji wa ubora wake.Ilipaswa elimu ya msingi iwe mpaka form four sio darasa la saba. Hii itasaidia kina Feisal wengi zaidi
Sijaelewa hii. Baba yake aliongea nini kuhusiana na hili?Amwombe msamaha baba yake. Baraka na laana hutoka kwa wazazi. Nilivyomsikia baba yake, kupitia vipanda vya video vilivyokuwa vikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, akijibu tuhuma za kula ugali na sukari ni kajua mzee haheshimiwi siyo na mama wala mtoto.
Baada ya kuomba msamaha akae na YANGA aombe msamaha ili aweze kujadili namna ya kuachana nao kwa amani. Akumbuke YANGA ndiyo imemfanya kuwa maarufu na ukitaka kuwa nyota wa mpira Tanzania heshimu SIMBA na YANGA.
Yetu machoMimi nadhani TFF wangeanza utaratibu wa wanatoa semina elekezi kwa wachezaji wetu wa ndani kuhusu kujitambua, kutambua haki zao, kuheshimu mikataba yao, kuheshimu vipaji vyao, kuuchukulia mpira kama kazi badala ya hobby/mahaba!, namna gani wanatakiwa kuishi wakiwa kama wachezaji wa kulipwa, nk.
Kiufupi nilishangazwa na kauli za huyu mtoto za kusema hana mahaba tena na Yanga! Na ndiyo maana anataka kuondoka. Yaani kwake kuchezea timu fulani, basi lazima uwe na mahaba na hiyo timu! Hii siyo sahihi hata kidogo.
Dogo alitakiwa kutambua kwamba mpira ni kazi kama zilivyo kazi nyingine. Hata kama yeye ni shabiki wa simba, bado alitakiwa kuiheshimu Yanga! Maana ndiyo iliyo muajiri.
Na kama alikuwa na ndoto za kuchezea Simba, angesubiri mkataba wake uishe mwakani, halafu angeenda simba kama free agent! Na siyo kwa kutumia hii njia yake ya mkato.
Basi ataenda Simba kama Yanga amesha haribu na hana timu nyingine ya ku opt tofauti na hizo ulizotajaSidhani, maana kwa Tanzania, timu za mchezaji kuweza kisimama ni Simba na yanga tu, na yanga ameshaharibu tayari,
Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app