Feisal anatufundisha Moyo wa Mtu kichaka

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Ndio moyo wa mtu kichaka umeficha mengi sana mabaya na mazuri,meupe na meusi, damu na maji...nk

Hakika msemo huu pasipo na shaka Feisal ametuonyesha maana yake, nani aliamini Feisal yule aliyekua anashangilia kwa kuibusu nembo ya Yanga pamoja na kwenda kwenye Camera na Kuisema I LOVE YANGA.

Pamoja na yote hayo hutoamini leo Feisal anasumbuana na Yanga Pale Tff huku akiwa amejaza mawakili karibia watatu kweli maisha haya yanabadilika binafsi nakiri bado sijaona mengi kwenye hii dunia Ndio RAFIKI YAKO ANAWEZA KUWA ADUI YAKO AND VICE VERSA IS TRUE.

Feisal aliyepita kwenye Nyakati ngumu na Yanga anzia kipindi kile cha bakuli yanga ikipitisha, akitumiwa na Zahera kama namba 6 na kucheza rafu nyingi na kula kadi za njano nyingi tu leo yupo pale Tff akizozana na Yanga.

Nani alitegemea kijana wa Byuti Byuti angeleta Mikwara wakati Yanga ikijiandaa na gemu ngumu na Azam kama ni mawazo ya kijana hakika kijana ana misimamo ila kama kuna watu nyuma yake wana lengo katili sana na timu ya Yanga.

Wapo wanaoamini Yanga imeundwa kupitia Feisal hii nchi kuna mengi kuna wivu, husda, tamaa mbaya, uchawi...nk hapo unaweza kukuta ni kakikundi cha watu wenye pesa zao wameungana kwa lengo la kuikomoa Yanga na kuirudisha nyuma bila kuwaza either wanamwaribia dogo au wanamsadia.

Kiuhalisia Yanga ni Taasisi Kubwa, Yanga ni Serikali kwanini Yanga ni serikali kuna watu wapo tiyari kufa kwa ajili ya Yanga tena mkulima tu wa huko sitimbi ndani ndani,Yanga anamiliki wananchi wake walio tiyari kwa lolote lile ni ngumu Feisal kushindana na Yanga yeye kama yeye labda kama atakua kwenye upande wa haki tu kwa njia haramu labda hao wanaomtumia wana mpunga au Tff waamue kupindisha Sheria.

Yes hatukatai Feisal alikua mchezaji muhimu Yanga lakini jiulize tangu ameondoka Yanga imepoteza michezo mingapi ? Feisal kapandisha kiwango miaka hii miwili ya Nabi baada ya kumtoa namba 6 na kumsogeza mbele na pamoja na kuzungukwa na wachezaji wazuri sisemi vibaya ila bado alikua na mengi ya kujifunza.

Bado hajawahi mchezaji wa kutegemewa ndio maana hata kwenye timu ya Taifa bado hana namba ya kudumu na hata akicheza hamalizi dakika 90 ndio narudia bado alikua na mengi ya kujifunza.

Na huu ndio ulikua wakati sahihi wa kudai DAU KUBWA KWA NJIA STAHIKI NA SIO ALIZOTUMIA YEYE WENYE LUGHA YAO WANASEMA JANJAJANJA MJINI, bado alikua na uwezo wa kukaa na timu ya Yanga na kuzungumza.

All in all yote heri kama kijana anaona njia aliyotumia ni sahihi its ok ila ni vema angeondoka na baraka za wazee nakumbuka kisa cha Maicon wa Brazil huyu jamaa alitakiwa kusajiliwa na timu moja ya italia kutoka timu ya Ufaransa Barcelona wakahijack ndege iliyombeba na kumshusha pale Nou camp kwa kifupi maisha ya jamaa Barca yalikua magumu sana.

Kijiji kisicho na wazee usiishi.
 
Tumeyasikia ya Feisali, tunataka tuyasikie na ya upande wa Yanga afu msimuliaji awe ni Feisali

Jaribu ku assume kama ndio Feisali anaharibu kuelezea changamotp za Yanga zilizofanya mpaka hayo yote yakatokea
 
Yanga ya Said wa Gsm Ina mazuri lakin ina mapungufu mengi sana kiutawala, na kimsimgi wapo kiujanaujana na usela mwingi Sana ktika Mambo ya msingi...!!. Ndio Fei anaweza akawa asiwe sahihi au sahihi lakini mbona kuna muendelezo wa matukio yanayofanana??, Morrison Sasa Fei na kwa mtazamo wakishabiki utaona yanga ndio ina haki lakini kumbe n propaganda na utoto!!.
Ni aibu kwa timu kubwa Kama yanga kuhangaika na mchezaji ambaye replacement yake kwenye kikosi ipo na anaweza sahaulika ndani muda mfupi Sana, viongozi wetu wajifunze kilibali na kuachana na Mambo ambayo wamekosea.
 
Kama feisal hana impact yoyote kwa yanga toka alipoaga kwanini mnaendelea kumng'ang'ania? Si mumuache akatafute maisha sehemu nyingine!
 
Tumeyasikia ya Feisali, tunataka tuyasikie na ya upande wa Yanga afu msimuliaji awe ni Feisali

Jaribu ku assume kama ndio Feisali anaharibu kuelezea changamotp za Yanga zilizofanya mpaka hayo yote yakatokea
Mambo ya tanzania yana dhuluma sana, kila nikimkumbuka kabwili huwa nahisi kuna mengi tusiyoyajua kwa toto.WATANZANIA SISI WABAYA SANA KWENYE HAKI HASA KWENYE KUNDI PAKIWEPO WANASIASA.
 
Yanga ni utopolo kama wanavyoitwa utopolo,ni ajabu hawamuongezei mshahara bali wanamlilia
 
Swala la Feisal na Morrison hayafanani labda umepewa wrong information
 
Acha maneno mengi.. watu wanaangalia hela.

We unadhani akizeeka atakula yale mashuti.. au unadhani atazeeka na zile jezi za yanga anazozibusu?

Pesa ndo kila kitu.. yaani yeye anawafurahisha bure tu... kama vile mapenzi ya mshumaa kumulikia wengine?
 
Yanga nao kwa mambo ya kiswahili Swahili hawajambo

"Kama mtu hakutaki mwache aende zake USIMBAKE" -Afande Sele.

"Kulazimisha PENZI ni hatari na ni sawa na kulazimisha fani Kisha unaleta utani"-Afande Sele.
 
Na wakati ukisema hayo nakukumbusha, mbinu anayoitumia FEI kutoka UTO ndiyo mbinu hiyo hiyo ilitumiwa na UTO kuwachukua GADIEL MICHAEL na SURE BOY... toka Azam, tofauti ni kwamba wote hao wawili Azam haiutaka kuwadai Fidia huku Sure Boy akipewa Option ya kurudi Chamazi km yatamshinda huku aendako!

KARMA is a Bitch
 
Yanga ni nn? Ni viongozi ambao walitakiwa kuboresha maslahi ya mchezaji? Au Yanga ni zaidi ya viongozi? Fei inawezekana hana tatizo na Yanga, ana tatizo na sehemu ndogo sana ya Yanga iliyotakiwa kutambua mchango wake kwa vitendo. Inawezekana kabisa kabla halijatoka nje ameshalia sana na viongozi wa Yanga bila mafanikio.
 
Swala la Feisal na Morrison hayafanani labda umepewa wrong information
Haina utofauti, yote tatzo ni mikataba na sio kingine... Kama mazingira ya kimkataba yasingemruhusu Fei kufanya hivyo Wala asingefanya. Hata yeye anawashauri wa sheria, katika hili nina 90% yanga itadondokea pua..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…