Feisal Salum anatafuta pesa za penati baada ya kushindwa

Feisal Salum anatafuta pesa za penati baada ya kushindwa

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
2,345
Reaction score
6,970
Iko hivi, Feisal Salum na Wakili wake wakiwemo wanaomdanganya wanafahamu kabisa huko CAS hawezi kushinda kwasababu mara nyingi CAS wao hupitia sana sana hukumu iliyotolewa na shirikisho la mpira Tanzania, hivyo siyo kwamba hela ya kuendeshea kesi milioni 60 hawana,hizo zipo.

Kinachofanyika hao washauri wake wamemwambia ajitutumue aende CAS ili kuonyesha yuko serious wakati yeye mwenyewe anafahamu kabisa hawezi kushinda, hivyo wamemshauri akielekea huko Yanga na Umma wa Watanzania wataamini kabisa hana kosa, sasa wanajua kabisa hawezi kushinda na ndiyo maana anachangisha mapema fedha za malipo kama adhabu ya kuendesha kesi hiyo huko CAS.

Hivyo kiasi hicho kitakapopatikana atakiweka ili kusikilizia upepo wa CAS ikionekana ameshindwa kama ambavyo anafahamu atazitumia hizo hela kulipia malipo hayo ya kuendesha kesi kama adhabu;Hela ya kufungulia kesi anayo, anachotafuta hapo ni hiyo hela ya fidia ya kushindwa kesi kama alivyoshauriwa na washauri wake.

Wamemwambia bila kupeleka Kesi huko CAS itaonekana amekubali kwamba ndiye mwenye makosa hivyo wamemjaza aende hivyo hivyo ili kuonyesha kwamba alipambana wakati akifahamu kabisa hawezi kushinda.

NB: MPUMBAVU HUDEKEZWA NA WAPUMBAVU, SIWEZI KUMCHANGIA KWASABABU NITAKUWA NADEKEZA MPUMBAVU.
 
Hayo ni maoni yako, Dogo achangiwe akapambane na hili genge la wahuni linaloundwa na baadhi ya watendaji wa TFF na Yanga

Binafsi namchangia.
 
Iko hivi,Feisal Salum na Wakili wake wakiwemo wanaomdanganya wanafahamu kabisa huko CAS hawezi kushinda kwasababu mara nyingi CAS wao hupitia sana sana hukumu iliyotolewa na shirikisho la mpira Tanzania,hivyo siyo kwamba hela ya kuendeshea kesi milioni 60 hawana,hizo zipo.
Mtoto umuleavyo..............................
 
Hayo ni maoni yako, Dogo achangiwe akapambane na hili genge la wahuni linaloundwa na baadhi ya watendaji wa TFF na Yanga

Binafsi namchangia.
Hata mchange, bado hamna uwezo wa kuzipata hizo milioni 50. Mnapoteza tu muda.
 
Dogo anaamin hawez kushinda huko,sasa anachotaka kufanya ni kuchezea hela za watu hata akishindwa asiumie maana pesa sio zake
 
Wacha tumchangie dogo kwani nikitoa elf 5 kuna ubaya gani hata kama akitumia kuhonga malayq hiyo hela mbona ni ndogo sana
 
Makolo ndiyo wanamchangia...sisi wananchi tunamwambia atumie zile 112m alizotaka kulipa yanga na atumie hela ya mshahara anayoirudisha yanga.
 
Back
Top Bottom