Feisal Salum Hawezi Kurudi Kwenye Ubora Wake Tena.

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Leo nimepata fursa ya kushuhudia huyu Kijana akicheza dakika zake 13 hapa Misri.

Kwa jicho langu la kiufundi huyu dogo ili acheze vizuri anahitaji hamasa sana hasa kutoka kwa mashabiki. Pia ni aina ya wachezaji wanaopenda kuzungumzwa ili afanye vyema kiwanjani.

Huyu dogo kamwe hatoweza kurudi katka ubora wake hata acheze timu yeyote ile hapa Afrika, labda akipata fursa ya kicheza mpira nje ya nchi ndipo atapata fursa ya kunolewa upya.

Yaani ni aina ya wachezaji kama Chama. Ili afanye vyema ni lazima mashabiki na waandishi wa habari wamsifie na kumzungumza kila wakati.


Licha. Ya fitness routine alizokuwa akifanya kipindi hayuko kambini na timu yake Yanga SC, bado anaonekana kuna kitu anakosa.

Unaweza ukamsaidia arudishe fitness yake ila ni ngumu saana kurudisha psychology yake ktk njia sahihi.

Dogo keshapotea.

Hata national team call up ilikuwa ni kwasabbu ya yule mpemba morroco aliyependekeza jina lake kwasababu za kiuzanzibar tu...Hakuna kocha mwenye leseni iliyo shiba anaweza muita feisal.

Kipaji kimepotea, ila kama taifa yatupasa tushukuru Mungu kwa kutupatiaMudathir Yahya.
 
Hawezi kupotea acha uchawi. Dogo leo kacheza vizuri unfortunately kapata muda mdogo. Hii Stars aongezwe Tshabalala, Kapombe na Kibu D kazi imeisha.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Hapana, mtoa mada amesema ukweli dogo ni mzito hata kucontrol mpira ni shida. Akicheza namba 6 au 8 atatuchomesha sana. Ona wenzake akina Muzamiru walivyo flexible mpaka raha. Kuhusu wa kumwongeza ni Kapombe tu wengine hao hawana nafasi kwa sasa.
 
Amijei wamemdanganya sana utopolo......Anaua kipaji chake.
 
Chomoa kwanza mwiko huko Nyuma,, una washwa washwa sana, ukaona thread haiwezi kukamilika mpaka umtaje mume wenu Chama,, anyway dogo sio kama atapotea bali ni wewe ndo unayetaka apotee,, Luc eymael aongezewe ulinzi popote alipo
 
Mimi kanifurahisha novatus dismas kiraka kaitendea haki full back ya kushoto ila fei toto alichelewa kuingia ground naamini Yuko fit Bado kama game ijayo ataanza mudatiri anakaa sana na mpira sehemu yakutoa pasi atoi
 
Nilichogundua Mwalimu anataka timu iwe ngumu sana kwenye kuzuia yani kusiwe na mtu mvivu na anapenda mabeki wote wawe wanaruka kusaidia kuokoa mipira ya vichwa, viungo wa shoka wanaoweza kugongana muda wote,
.

ila bado nahisi Shomary Kapombe ana umuhimu sikwamba Job amecheza vibaya la hasha nikua kunahitajika mtu ambae yuko comfortable na eneo lake ili kutengeneza balance nzuri ya timu.
 
Hawezi kupotea acha uchawi. Dogo leo kacheza vizuri unfortunately kapata muda mdogo. Hii Stars aongezwe Tshabalala, Kapombe na Kibu D kazi imeisha.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Taifa Stars ingefungwa leo wangesema kwasababu hakina nanihii waliachwa.

Ebu ona kule nyuma Manula alikuwa analindwa na Job, Mwamnyeto na Baka, alitulia tulii kwa raha zake
 
kaanguka mara 25
 
Feitoto ame nenepa kwakua Hakua katika mpira wa Ushindani Kwa muda mrefu, Ili kumsaidia apunguze mafuta yaliyo zidi kwanza.
Kulazimisha kumchezesha akiwa na uzito mkubwa kunaweza ku msababishia majeraha ambayo yatamweka nje Kwa muda.
 
Hapana, mtoa mada amesema ukweli dogo ni mzito hata kucontrol mpira ni shida. Akicheza namba 6 au 8 atatuchomesha sana. Ona wenzake akina Muzamiru walivyo flexible mpaka raha. Kuhusu wa kumwongeza ni Kapombe tu wengine hao hawana nafasi kwa sasa.
Hilo huwa ni kawaida kwa mchezaji yeyote anapo kaa nje ya pich kwa muda mrefu akicheza mechi mbili anarudi kwenye hali ya kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…