Feisal umemalizana na Uongozi bado hujamalizana na mashabiki wenye hasira kali juu yako

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Mara zote mchezaji anapoondoka Yanga kihuni na kwa ngebe na kebehi nyingi huwa mwisho wake ni mbaya sana. Tunarejea habari za wakina Frank Domayo, Gadiel Maico, Ibrahim Ajibu, na wengine kilichowakuta wanakijua mpaka sasa wamepotea kwenye ramani ya soka.

Kwa maana hiyo waombe msamaha wanachama na mashabiki wa Yanga kwa maneno ya ovyo uliyokuwa unayatoa vinginevyo Kamati ya Ufundi aitokuacha salama!
 
Mkojani hana muda na wenye hasira Ana deal na washika karatasi zake.
 
Acha usenge wewe sasa unamtisha nani? mrogeni basi, nonda aliondoka yanga vizuri? mbona alitoboa hadi ulaya?
 
Kwa hesabu za haraka mkataba wa feitoto na azam wa miaka(4) mil 470.. ni sawa na mshahara wa 6,337,830... kwa mwezi!. Nett Pay.

Chukua mil 470/48-Nssf-PAYE Unapata hiyo amount... Kaacha fan-base kubwa kwa deficit ya 2 million tu!
 
Katika hiyo list yako mbona hujamuweka Morrison?

Rekodi zinaonesha watu wengi waliokuwa kwenye mgogoro na Yanga na kufanya mashabiki wamchukie mtu huyo.

Basi mara nyingi mtu huyo inakuwa ni swala lepesi sana kukaribishwa tena kwenye Club hiyo.

Bernard Morrison alikuwa mfano, kawatia hasara ya muda na pesa, nakumbuka siku ya mwananchi Nugaz alimtaja Morrison kwenye list ya wachezaji wakati tayari kasepa.

Lakini kunaye Manara ambaye huyu ndio alikuwa mwiba kwenu, kwa mtu ambaye alikuwa anaona jinsi mashabiki wa Yanga wakichukizwa na huyu mtu mpaka kufikia hatua wanamu edit akiwa amevaa shela, ni ngumu sana kufikiria huyu mtu anaweza kupokelewa vizuri na hiyo Club. Lakini imewezekana.

Sasa ndio iwe Feisali?
 
Binafsi kutokana na umri wake, uelewa wake, jina lake (Fei Toto), nk. Nimechagua kwa moyo mmoja kabisa kumsamehe. Kamwe sitakuwa na kinyongo naye. Awe na safari yenye heri kwenye maisha yake mapya. Naamini pia amejifunza kitu ndani ya hii miezi 6 aliyoitunishia msuli, taasisi kubwa kama Yanga.

Akimbuke pia wapo wachezaji wenzake wengi tu walioenda huko Azam wakitokea Yanga, na mwisho wa siku wameishia tu kuchemka.


Enzi hizo kulikuwa na Frank Domayo!! Akiwa katika kilele chake cha mafanikio pale Yanga, kiasi cha kuitwa chumvi aliondoka na kwenda Azam baada ya kuahidiwa dau nono! Leo hii, Frank Domayo yuko Namungo Fc! Tena hakuna hata shabiki wa Yanga anayemkumbuka.
 
Tuambie mchezaji gani wa Yanga aliyebaki wa enzi za hao unaowataja ana mafanikio.
Nsajigwa aliyezeekea kwenu yuko wapi, Ngassa aliyefanya upuuzi asiende kucheza nje yuko wapi na wengineo.

Kwanza Feisal wa visiwani hatishwi na kina Mzee Mpili hao.
 
Na yupo kwenye orodha ya kuachwa tena mwisho wa msimu hapo Namungo🤣🤣
 
Ndio Maana tulikubaliana kwamba Nyuzi nyingi Zina, ondikwa na MASHABIKI WA Yanga ni mbovu mno, UANDISHI mbovu, hoja 0

Kwani ukiwa kimya unapungukiwa nini unakuja kuleta Uzi hauna mbele Wala Nyuma!!!!!.

Umeambiwa Mchezaji atacheza yanga Maisha yake yote.

ACHA wachezaji wajitafitie Riziki.
MAISHA ya mpira ni mafupi mno.

FICHA UJINGA
 
eengineer aliwaita WALA MIHOGO na hamkufanya kitu sembuse huyu FE8SAL
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…