Feitoto ni mchezaji mzuri ila kwa sasa ni overrated

mwehu ndama

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,472
Reaction score
9,542
Binafsi nimeanza kumfuatilia Feisal kama mchezaji tangu akiwa JKU, na kwa kipindi Fulani kama ilivyo kwa wanamichezo wengi ,"Zanzibar finest" aliwahi kuwa katika ubora wa maisha yake (prime period) na hii ilikuwa misimu yake mitatu ya mwisho Yanga na walau ule wakwanza akiwa na azam FC .
Na katika ubora wake alikuwa akitumika kama central midfielder katika Yanga iliyokuwa ungaunga. Alikuwa energetic, combative, uwezo wa kucheza box to box, au namba kumi kulingana na mahitaji ya mwalimu.

Lakini baadae Nabi alimbadili nakumpa majukumu ya kudumu shimoni , na hapo ndipo ubora wake mkubwa uipoonekana .ila hii lichangiwa na nguvu kubwa za wachezaji waliokuwa pembeni yake , bangala ,aucho ,sure boy n.k.

Na hata alipofika azam FC msimu wake wakwanza alimkuta James akaminko,Adolf bitekego, na yahya zaidi wakiwa in Good form bila majeraha,kitu kilichompa urahisi wakufunga ingawa tayari alianza kuongezeka uzito na kuwa single zone player.

ila kwa sasa tunamuimba sana ,nakumtaja sana wakati ambao uwezo wake unashuka chini na sio kupanda tena . nafikiri Ile njaa yamafanikio aliyokuwa nayo hapo awali imeshaondoka na hii nikawaida kwa wachezaji wa kizanzibari kama ilivyo kwa wachezaji wakibrazil ambao mara nyingi uridhika na mafanikio na kuanza kuinjoy matunda Yao kabla ya muda mahususi wa kustaafu haujafika.
Ukweli nikwamba faila sufi Yuko chini ya kiwango , lakini sisi kama taifa tumeshachagua kumfanya superstar wa nchi ,hivyo nayeye anatembea na upepo
 
Ni mchezaji mzuri sana ni vile yupo kwenye Nchi mafanikio yetu ni kuchezea Yanga/Simba huyo dogo mpira anajua tena kipaji kama pana mtu anamkosoa Salum ajikite kwenye fani yake sio futbal..
Bro mpira sio kama kujua baiskeli au gari kwamba ukijiu umejua ,mpira ni juhudi pamoja na maarifa , unataka kuniambia kaizer chief au mamelod au wydad Casablanca hawan hiyo 500,000 USD yakumtoa Azam? Inshu nikwamba wabongo tunatanguliza utz badala ya uhalisia ,dogo mpira anajua ila amesharidhika na life ya Pemba Hana juhudi na ndio maana timu za nje zote zinamtema
 
Kaka Watanzania wengi hawafikirii kucheza nje au kufanya vitu nje ya Tanzania huyo salum angekua mganda,mkenya au Nigeria ungesikia Timu anayocheza tuna udumavu mkubwa sana hao kaizer wana nani pale wa anashika shika kama Salum..
 
Ndio point yangu ilipo , Hana juhudi , alikuwa na uwezo wakwenda cheza Hadi ulaya lakini kwa alipofika ,akisaink huu mkataba mwingine na azam FC , basi na mpira unaishia hapo. Anaridhika anarudi kula urojo
 
Feisal siyo Msuva wala Samata, ni Feisal, humu humu ndani juhudi zake hazijifichi. Na mpaka sasa maamuzi yake ya kisoka ni sahihi na yamemlipa na huu mkataba wake unaofata utamlipa.

Kuhusu kupata timu nje huenda hajataka na sio hatakiwi.
 
Nyambafu kweli wewe, kwahiyo unaposema Feisal ni overrated player unahisi hao wenzako haitowauma, bado itaendelea kuwauma.
 
Ndio point yangu ilipo , Hana juhudi , alikuwa na uwezo wakwenda cheza Hadi ulaya lakini kwa alipofika ,akisaink huu mkataba mwingine na azam FC , basi na mpira unaishia hapo. Anaridhika anarudi
Huwezi kwenda ulaya ukiwa 27+ ukapata timu na kufanya vizuri.

Inatakiwa 17 yrs ikukute ukiwa huko tayari.
 
nakubaliana na wewe 100%,, Sijui simba tunamsajili anakuja kuongeZa kitu gani,,

binafsi nimekuelewa, ile mechi ya jana sijui imekuaje hadi kama man of the match 😆
 
nakubaliana na wewe 100%,, Sijui simba tunamsajili anakuja kuongeZa kitu gani,,

binafsi nimekuelewa, ile mechi ya jana sijui imekuaje hadi kama man of the match 😆
Ukisikia bahati ndo Ile.Nilitegemea Mudathir apewe maana aliubonda mno
 
Feisal siyo Msuva wala Samata, ni Feisal, humu humu ndani juhudi zake hazijifichi. Na mpaka sasa maamuzi yake ya kisoka ni sahihi na yamemlipa na huu mkataba wake unaofata utamlipa.

Kuhusu kupata timu nje huenda hajataka na sio hatakiwi.
Kuna tetesi kuwa Feisal amechukuliwa na Nabi kimya kimya, atajiunga na Kaizer Chiefs baada ya mashindano ya CHAN 2024.
 
Reactions: Tsh
Kwa kweli aisee....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…