Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Picha> Mbunge Felista Njau akitoa hoja bungeni
Felista Njau, Mbunge wa viti maalum akiwa Bungeni leo ametoa mchango wake kuhusu bajeti huku akisisitiza kuwa bajeti imeacha kipengele muhimu cha Diplomasia ya uchumi katika kufafanua jambo hili alisema:
"Katika bajeti sijaona kipengele muhimu nacho ni diplomasia ya uchumi, Rais Samia Suluhu ameonekana kama mtu wa kutoa pasi za mwisho za kufunga katika eneo la diplomasia, hivyo wanapaswa wapatikane wafungaji. Kila mtu acheze kwenye nafasi yake".
"Wakati tukiimba Royal Tour inaleta matokeo, ni lazima twende kwenye diplomasia ya uchumi kujiuliza namna gani tutapata watalii zaidi, wawekezaji na kufungua fursa mbalimbali kwa Taifa letu, katika hilo Rais Samia
amecheza nafasi yake nasi tucheze nafasi zetu".
"Katika balozi zetu hakuna kitengo cha habari, ukiangalia blogs mbalimbali za Wizara na mitandao ya kijamii ya balozi huoni wakitangaza bidhaa zetu. Tunahitajika kujipambanua kama Watanzania, na sio kusubiri mtu mmoja atangulie mbele na kisha sisi turudi nyuma".
Nini mtazamo wako kuhusu hoja zilizotolewa na Bi. Felista Njau