Felix Tshisekedi anapoteza DR Congo

Felix Tshisekedi anapoteza DR Congo

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Sijui kama felix anakomboa Kongo au anazidi kuipoteza Congo.

Wakongomani tulimtukana Katumbi kwa kusema sio mkongomani sijui maneno mengi alivyosema kuna ya kuachana na vita hivi tujenge kwanza jeshi imara.

Ambalo litakuwa na uwezo wa kupambana kuliko kushirikisha majeshi mengine ya nchi zingine kuja kutusaidia maana katika majeshi hayo kuna baadhi yao sio waamanifu na wananchi hawana imani nao.

Wengi walimtukana na kusema sio mkongomani sijui yeye ndo kiongozi wa M23 walimpa majina yote mabaya
Haya leo tuko wapi.

Kwanini tunaandana sasa kudai jeshi la Kenya litoke ndani ya nchi yetu. Si mlisema wanakuja kutusaidia waache watusaidie tu.

Kumbukeni hata lorent kabila ambaye alituletea upumbavu huu ndani ya nchi yetu alishirikiana na nchi jirani kwa makubaliano yao leo hii tunalipa kwa damu.

Uhuru wakongo utapatikana kwa wakongomani wenyewe tukiwa na kiongozi mwenye akili nzuri ambaye sio mlalamikaji kama felix. yule kagame tunamuondoa madarakani kwa dakika tu.

Tukiachana na ushabiki Katumbi michezo hiyo anaijua vizuri kama Kabila alimuogopa Kagame ni nani?
 
Wakongomani ni nini wanachopigania lakini, nimewahi kutumiwa video za watu wanavyouana Congo huwezi kutizama mara mbili hata Boko Haram hawafai.

Tshisekedi aliingia madarakani kwa ahadi ya kumaliza huu unyama lakini ameshidwa kabisa na sasa ni vyema asichaguliwe tena kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

Labda wampe Bw. Martin Fayulu ambaye ndiye aliyeshinda uchaguzi wa mwaka 2018 kabla ya kufanyiwa hila na Kabila.
 
Back
Top Bottom