Ferdnand Ndikuriyo (Chuma cha Chuma) ashindwa tena masharti ya dhamana, arudishwa Rumande

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
1732024371224.png
Mshtakiwa Ferdnand Ndikuriyo (27), maarufu Chuma cha Chuma ameshindwa kutimiza masharti matano ya dhamana ikiwamo kusaini bondi ya Sh10milioni na wadhamini wawili raia wa Tanzania wanaotambulika kisheria watakaosaini bondi ya Sh10 milioni kila mmoja.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetupilia mbali ombi la dhamana ya mshtakiwa, lililowasilishwa na Serikali badala yake imempa masharti mshtakiwa huyo, ambayo ameshindwa kuyatimiza.

Ndikuriyo, ambaye ni msanii wa muziki na raia wa Burundi anakabiliwa na shtaka moja la kuwepo nchini bila kuwa na kibali.

Uamuzi huo umetolewa na leo, Novemba 19, 2024 na Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, baada ya kupitia maombi yaliyowasilishwa na upande wa mashtaka na ule utetezi kuhusiana na kuzuia dhamana ya mshtakiwa huyo.

PIA SOMA
- Ferdnand Ndikuriyo (Chuma cha Chuma) afikishwa Mahakamani, akabiliwa na Kesi ya kujibu
 
EAC bado tuna safari ndefu sana😎
 
Kutakua na kitu zaidi ya kuwepo tu nchini..labda jamaa ameshtukiwa alikuja na plan hatarishi
 
Back
Top Bottom