Fernandinho

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
FERNANDINHO KATIKA NAFASI YA BEKI ANA FAIDA GANI NA HASARA GANI !

Pep si mara ya kwanza kumchezesha kiungo wake katika nafasi ya ulinzi hii ni mbinu ambayo wengi humulikia hasara zaidi ya faida!Kama ripoti ya skauti nitamilikia baadhi ya faida Manchester City wanazipata kwa kumtumia Fernandinho katika nafasi iyo.

Guardiola anaanza kutengeneza kuanzia nyuma,hivyo anahitaji mchezaji mwenye upeo wa kuona mbele ambapo wachezaji wengi huwa ni viungo,Fernandinho ni kiungo kwa kuzaliwa hivyo ule upeo unasaidia katika kutengeneza nafasi (spaces) , na nafasi ya kucheza (position play ) na kuona wachezaji uwanjani.

Fernandinho kuwepo kama beki kuna msaidia Guardiola kuwa na mchezaji ambaye anajua mahali pa kupeleka mipira wakati wa kutengeneza (playermaker at the back) mfano ; Abumeyang alikosea katika mchezo wa juzi (Arsenal) katika kukaba juu (high pressing) alienda kukaba badala ya kudeny space hivyo kuachia mwaya aliopeleka mpira na kuipita kiungo ya kati na mpira wa kupitishwa kwa Jesus aliyemimina grosi ya chini na Kelvin De Bruyne akaachia mkwaju pembeni juu na kuiandikia Manchester city bao hapo Fernandinho alitumika kwenye ( short ending sequence involvement) ikiwa yuko katika nafasi ya ulinzi.

Fernandinho anajua jinsi ya kupiga (tactical foul) kucheza rafu ya kimbinu wakati Manchester City wanacheza wana ushujaa wa mchezaji anayeweza kusimamisha timu wakati wakifanyiwa (transition) hivyo kupunguza hatari ya shambulio la kushtukiza.

Fernandinho anatoa misaada miwili kwa wakati mmoja katika eneo la katikati,anasaidia kuongeza idadi ya namba (numerical superiority ) ikiwa wakati wa (kubuild up ). Licha ya faida za Fernandinho kuongeza nguvu katika eneo la kati wakati wa kutengeneza (build up play ) , ukweli ni kuwa katokana na miaka 34 ile kasi imepungua sana hivyo hushidwa kushikilia baadhi ya wachezaji wenye kasi (mfano wa Vardy na Traore ) , Fernandinho bado si kiasi cha mzoefu katika eneo hilo kuna muda anasahau kwenda kukaba ama kutulia na kuvutia pumzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…