Ferrari wamezindua Ferrari F80, inayouzwa Tsh Billion 10.5 tu! Na ata kama unayo iyo pesa, huwezi nunua kwasababu yameshauzwa yote!

Ferrari wamezindua Ferrari F80, inayouzwa Tsh Billion 10.5 tu! Na ata kama unayo iyo pesa, huwezi nunua kwasababu yameshauzwa yote!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Ni tabia ya Ferrari kuzindua racing-inspired supercar kila baada ya miaka 10, na last time 2013 tuliletewa Ferrari LaFerrari, na sasa mrithi wake amefika.
images (4).jpeg

Ferrari F80 ni supercar. Ni racing car. Ina DNA za Ferrari 499 na SF

NB: Ferrari 499 ni hypercar iliyoshinda LeMans mara mbili. Na SF (Scuderia Ferrari) ni category ya magari ya F1 Ferrari team.

Kwahiyo F80 ni street version ya hayo magari. Hadi sasa ni most powerful production car kutoka kwa Ferrari, ikija na 1200 hp, ikiwa na V6 engine (yenye cc 3,000 inayotoa 900 hp) na electric motors mbili (zinazotoa jumla ya 300 hp).
images (9).jpeg

Ikumbukwe pamoja na kwamba F80 ni Hybrid, ila haiwezi kutembea EV mode ata sentimeta 1, pamoja na kua ina battery la 2.3 kWh. Hizi motors ni kwaajili ya kuboost performance, sio mambo ya fuel economy.
images (3).jpeg

Kwa muonekano, F80 ina butterfly doors zinazofunguka kuelekea juu kwa showoff.
images (5).jpeg
images (6).jpeg

Kwa ndani, F80 haina mbwembwe za kibishoo kwasababu iko focused on driving. Ndio maana hauoni infotainment screen na seat ya abiria wa mbele haina comforty tulizozoea kwenye magari ya siku hizi.

images (11).jpeg

Pamoja na kwamba ni racing car, ila wameweka adaptive cruise control, active rear wings (zinaweza kupanda na kushuka pamoja na DRS), diffuser, front wings na flat underbody ambavyo vinamsaada sana kwenye racing kwani vinatoa total ya ton 1 ya downward force ukiwa speed ya 250 km/h.
images (10).jpeg


Kununua hii gari labda usubirie used. Maana Ferrari wametengeneza 799 tu ambazo zote tayari zimalipipiwa na matajiri wenzako.
images (7).jpeg

Ikumbukwe hawa jamaa Ferrari ikija kwenye issue ya kuuza magari yao wako serious sana.

Mfano:

Ferrari hawakuuzii gari jipya kama haujawahi kumiliki Ferrari, ata uwe tajiri kiasi gani.

Wanachofanya wanatuma invitation kwanza kwa wamiliki wake kuwaambia kama wako interested kununua model mpya. Kwakua mara nyingi wanakua ni matajiri sana, wanajibu yes ndio maana unakuta gari imetangazwa this week tayari imeisha sokoni.
 
Back
Top Bottom