Festo Sanga wewe ni mbunge mzuri sana usijiingize kwenye mambo ya Makamba yatakuchafua

Festo Sanga wewe ni mbunge mzuri sana usijiingize kwenye mambo ya Makamba yatakuchafua

Mtumishiwetu

Senior Member
Joined
Jul 13, 2022
Posts
196
Reaction score
346
Mbunge wa Makete, Festo Sanga achana na mambo ya kushabikia mambo yasiyoeleweka ya Waziri wa Nishati, Januari Makamba yatakuharibia sifa uliyoanza kuijenga kwa wananchi wako.

Jana wakati mjadala unaendelea kuhusu gharama za kuunganisha umeme, ulipost kwenye akaunti yako ya Instagram ukiituhumu ITV kupotosha maudhui ya mazungumzo na Waziri Makamba.

Kama hiyo haitoshi uliweka bayana kwamba unaamuunga mkono Rais Samia na kumuunga mkono Waziri Makamba, lakini baadaye uliamua kuifuta post hiyo kwenye akaunti yako.

Kitendo cha kufuta post yako utakuwa umegundua ulifanya makosa makubwa kujinasibisha na Waziri ambaye amesajili ugomvi mkubwa na umma wa watanzania.

Nakusihi kama unataka kuwa mwanasiasa mkubwa siku za baadaye fuata maagizo ya Makamu Mwenyekiti wa CCM, Komredi Kinana aliyewataka wabunge muwe wakali kuiwajibisha Serikali kwenye mambo ya wananchi.
 
Back
Top Bottom