Mini nadhani kuchukua muda mrefu au mfupi ndani ya chumba cha usaili hiyo sio hoja. Kinachotakiwa ni uwezo binafsi wa mtu kujieleza na kujibu kile ulichoulizwa. Tatizo letu sisi wabongo utataka kuonge vitu vingi sana ili uonekane unajua sana ambapo katika maelezo yako hayo wewe mwenyewe unajitengenezea maswali mengi ambayo ukiulizwa uanaanza kujiuma uma tu. Kingine ni kutokujiandaa kwa usaili. Ni kosa kubwa sana kwenda kwenye usaili bila ya kujiandaa vya kutosha. Utakuta mtu hata jina la mahali anapoomba kazi hawezi kulitamka sawa sawa wala hajui lolote kuhusu mahala pale.
Hivyo basi kinachotakiwa kwanz akabisa ni kujiandaa vya kutosha kwa maana ya kuifahamu kazi unayoomba pamoja na shirika au kampuni lile unaloomba kazi. Cha pili ni kujiamini na kujibu maswali yale uliyoulizwa. Tatu, kuwa na mwenekano mzuri kwa maana ya mpangilio wa mavazi yako. Nne, ni weledi katika lugha na kama kitu hujui au hujamuelewa anayekuuliza usisite kumuuliza ili akufafanulie kile anachokuuliza. Usijibu maswali kwa sababu tu ya woga au hofu kwamba utaonekana hujui, kama hujui sema hilo lisijui. Jmabo la mwisho ni mshahara usipende sana kutaja kiwango kama huna hakika na nagzi za mshahara za mahali hapo. Unaweza ukataja mshahara kumbe mshahara huo ni wa ngazi ya mkurugenzi wakati wewe unaomba nafasi ya afisa wa kawaida tu. Zaidi ya yote tafuta habari za kutosha za mahali unapoomba kazi ukianzia na kazi unayoomba, mazingira utakayofanyia kazi, mishahara na marupurupu yao n.k. Nina imani ukizingatia hayo yote utafanikiwa katika usaili wako.