labda wanamsingizia. Au anajiami. kosa la mchumba wako sio lako. Muoe hivo hivo kama umempenda na msapoti tu basi. Mie nilikuwa na wifi mwenye tabia ya umbea ushangingi na ugombanishi.
Kaka yetu mkimya sana, watu wakiogopa kumuambia. Na hata wakimuambia yeye wala hamulizi mkewe, kaka yetu alikuwa haweki akilini mambo kama hayo.
Kuna siku ugomvi ukaja hadi nyumbani kwa kaka, ngumi mtu, heheh. ile kaka anatoka nje tu wanawake wakakimbia na kumuambia yule wifi mumewe akitoka tu watakuja kumkomesha. Wifi akasema njoeni tu hawaogopi. wakarushiana maneno. kaka alipouliza, akasema mijitu mingine mishenzi.
wifi alipopata mimba ndio akatulia, akawa mpole. Alipo zaa marafiki zake wakamuambia anuka mikojo na kapitwa na wakati. akamuambia kaka wamie sehem ingine kuepusha shari. Sasa wifi yetu sasa sio yule wa zamani, sasa kakomaa akili na wanaendelea kuishi pamoja na mumewe vizuri tu.
mchumba ako, ujana unamuangaisha, ila kuna siku hiyo tabia ataiacha. Jifanye kama haujui, na jifanye haikuhusu wewe. Hao watu wanao kulalamikia waambie ni bora wamalizane wenyewe na huyu dada. Husifuatilie sana mambo ya wanawake, na inawezekana pengine wanamzushia tu mwana wa watu, na analipiza kisasi kwa kuwachonganisha. mtu hawezi tu kuwachonganisha watu bila sababu, mie naona labda mchumba wako anajiami kwa jambo fulani hapo. Muulize mwenyewe kwanini anafanya hivo, atakuambia.