Fid q, afande sele nani zaidi? Fainali leo hii!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363



Na GPL Ripota
Miamba inayofanya makubwa katika Muziki wa Kizazi Kipya nchini, Farid Kubanda a.k.a Fid Q na Seleman Msindi a.k.a Afande Sele, ndiyo inayokamuana katika Nani Zaidi wiki hii...

Hawa ni wakali wa Bongo Fleva ambao walianza game kitambo, lakini walikubalika zaidi kuanzia miaka ya 2002 na kuendelea.

Wana pini kibao ambazo ziliwafanya waendelee kuwa kileleni, lakini songi kama Mwanza Mwanza lake Fid Q na Kingdom wake Afande Sele ambaye pia aliwahi kuwa Mkali wa Rymes zimekaa vizuri ile mbaya.

Sasa tuambie, kwa maoni yako, kwa jinsi unavyowafahamu wakali hawa, unadhani nani anastahili kuwa mbabe wa mwenzake? Toa maoni yako hapo kwenye poll, juu kulia.
 
Poll mbona haionekani?
 
Unapotaka kutaja wakongwe ktk muziki huo basi hao uliowataja wote ni uharo tu...
Ili nikuelewe labda ungewataja
Saleh jabir
Sugu
Sos B
Ebwana dah ebwana dah Saigon
Balozi
Profesa J
Na makundi machache.

Kuna visanii vinajiita vikongwe wakati vimekuja na boti ya Clouds FM...
 
Unapotaka kutaja miamba ktk muziki huo basi hao uliowataja wote ni uharo tu...
Ili nikuelewe labda ungewataja
Saleh jabir
Sugu
Sos B
Ebwana dah ebwana dah Saigon
Balozi
Profesa J
Na makundi machache.

Kuna visanii vinajipa umwamba na ukongwe wakati vimekuja na boti ya Clouds FM...
 
Kwa sasa FID Q zaidi ya Afande
 
Wote wako poa kwa yangu maoni,
Afande sele punguza mchupa mwana utashupa
 


FID Q AMFUNIKA AFANDE SELE

photos


Hatimaye msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Farid Kubanda a.k.a Fid Q amemfunika msanii mwenzake ambaye pia aliwahi kuwa mkali wa Rymes, Seleman Msindi a.k.a Afande Sele katika mpambano wa nani zaidi kimuziki, baada ya kujizolea asilimia 61 ya kura zote zilizopigwa na wadau kupitia mtandao huu pendwa duniani kote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…