Haumuui chura kwa kumtupa ndani ya maji
Ukinizuga kwa ulaji, nakupa fact kwa lugha ya kishkaji
Unataka vitu rahisi, mi' nawapa vitu halisi
Utata unamtaka ibilisi, na siyo bi kaka ka' Idris
Mr. Nice jua la utosi na mtaa unakiu ile mbaya
Hawamsupport, isipokuwa anawapromote aliowa-inspire
Wakati, ___ sio kama Mox, Stosh hakupaswa kumgwaya
Lakini, mzee bila noti ni zaidi ya Nyoshi akiwa vibaya
I didn't come this far, just to come this far
Siwezi sanda kama bikra hata nikiishi ki-star
Maisha hayakupi unachotaka ila yanakupa unachotafuta
Pesa sadaka, wazushi wanaivuta kwa ________
Binadamu wako wapi mnanitoa mie nsiwemo
Leo nawapa ofa ya mswaki afu kesho mnaning'oa meno
Oyoooo.. time is money nafasi haijali kuzuga
Wema anataka saa ya almasi zari anaujali muda
Washa sana nyasi, rasta ogopa fast futa
Wanashindwa kujinafasi kwa unafiki nafsi zinawasuta
Wabongo wa majuu hamna upendo, mnajigawa
Ubongo hauna miguu lakini skendo zina mabawa
Aliyemtia umasikini Afrika leo analia kwa yanayomsibu
Na hutangaza akimpa msaada kiasi cha kumtia aibu
Dunia siyo chafu ni chafu uchafu tukiutazama
Sumu ndani ya watu, na ndiyo hapohapo tunapokwama
Hawaamini kwenye kuunda Diamond au Kiba wawili
Wanachoamini ni kumshusha mmoja ili mmoja awe dili
Cha kupewa hakishibishi ukipewa lazima ukumbushwe
Dunia mwendo wa ngisi, kung'aa sio lazima star ashushwe
Ukiacha hisia zikuendeshe, kwa ujeuri utaishia kufeli
Sababu neno la ukweli sio zuri na neno zuri halina ukweli
Ntasahau vyote, milele ntamkumbuka aliyeniumba
Na daily ntakaa mkao wa pusha tu kama Umbwa