Fidia kwa waliopisha upanuzi wa uwanja ndege Msalato

Fidia kwa waliopisha upanuzi wa uwanja ndege Msalato

COMOTANG

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2021
Posts
2,131
Reaction score
1,821
Habari za jioni.

Kwa wanaohusika na malipo ya fidia ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato -Dodoma mtatulipa lini fidia hiyo miaka inakwenda ardhi na vilivyomo havituzalishii toka mlipohakiki mara ya kwanza mwaka 2018 ni miaka mitatu,

Sasa je, mtaongeza kiwango cha fidia au ndo mtatulipa senti kwa thamani ya mwaka 2018?
 
Msalato International Airport tuachane na Mambo ya kule Kanda pendwa
 
Ni hivi nyie mliopo serikalini mlipojua utajengwa uwanjwa wa kimataifa mkaamua kununua viwanja. Ili mlipwe fidia kubwa.

Serikali mpange fidia.
 
@ COMOTANG,

Unafuzi vigezo vyote kabisa kulipwa fidia tosha.

Wale walionunua baada ya matangazo ya kujenga uwanja wapangiwe bei za kulipwa ni kodi zetu.

Ndio watu wa Serikali. Walijua hivyo.
 
Kumbe uwanja wa ndege Msalato haujaanza kujengwa?
Nilijua tunasuniri kuufungua tuu
 
Nilikuwa nalisha familia pale, mwaka mzimaa sinunui nafaka za mahindi na mtama Wala mafuta ya Alizeti.
 
Kumbe uwanja wa ndege Msalato haujaanza kujengwa?
Nilijua tunasuniri kuufungua tuu
Wengine hatujalipwa mkuu walio lipwa Ni wale waliosahaulika kulipqa mwaka 2008 na walihakikiwa upya mwaka 2011/12 2019/2020
 
Kama hauna tija kwanini ujengwe? Kama una tija,mbona walifanya upanuzi ule wa mjini? Ndege ni zilezile tu,
 
Habari za jioni.

Kwa wanaohusika na malipo ya fidia ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato -Dodoma mtatulipa lini fidia hiyo miaka inakwenda ardhi na vilivyomo havituzalishii toka mlipohakiki mara ya kwanza mwaka 2018 ni miaka mitatu,

Sasa je, mtaongeza kiwango cha fidia au ndo mtatulipa senti kwa thamani ya mwaka 2018?
Ukilipwa mkuu usinisahau mnadani,nyama za mbuzi mkuu!
 
Subira yavita kheri... mngepiga kelele kipindi kilekile...
 
Kama ni hivyo wanasubiri Nini kulipa fadia? HIVI WABONGOLAND tuna tatizo gani?
 
Back
Top Bottom