Fidia ya hasara iliyosababishwa na mtandao wa Vodacom

Fidia ya hasara iliyosababishwa na mtandao wa Vodacom

cheze

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2011
Posts
501
Reaction score
330
Wanabodi,

Tangia Jumamosi tar.14 hadi Jumanne tar.17 mtandao wa M-PESA haukuwa unapatikana nchi nzima, hivyo basi kuna hasara kubwa iliyopatikana.

Kwa mfano mfanyabiashara anategemea kutimia M-pesa kupokea/kutima pesa iweze kutumika kibiashara na anategemea faida kwa mzunguko huo wa pesa kwa siku. Achilia mbali kampuni ya vodacom ilivyosema kuwa pesa za wateja zipo salama lakini wakumbuke kuwa hiyo pesa kwa siku 3 imekaa tu kwao bila kuiingizia faida kibiashara kwa jinsi ilivyotegemewa.

Ipo mifano mingi, kuna watu wamepoteza maisha yao wakitegemea kutoa pesa kwenye M-Pesa ili kulipia huduma za matibabu.

Je haya madai kisheria wahanga wanapaswa wafuate mlolongo upi?..
 
Back
Top Bottom