Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 31,009
- 60,629
Siku hizi wengi wanaingia kwenye mapenzi kwa sababu ya pesa, maumbo ama sura nzuri. Waoamini mapenzi bila pesa nao wanaongezeka kila siku kutokana na hali halisi hivyo siwezi kuwalaumu japo sikubaliani nao. Nnachojua mimi ni kwamba mapenzi hayanunuliki, kinachonunulika ni mahusiano.
Nwy nilikua nafikiria jinsi gani hivi vitu vitatu (pesa, sura na umbo) vinavyosababisha watu wasizingatie vitu ambavyo ndio misingi ya kuendesha mahusiano yenye faida kwa pande zote.
Kwasababu wanaume (sio wote) wanaamini kwamba mapenzi yananunulika, kishawishi wanachotumia kuwakamata wanawake ni pesa. Na wanawake wanatumia sura na maumbo yao.Pesa inatumika kufidia mambo ambayo ni ya msingi. Vile vitu vyote ambavyo havinunuliwi kwa pesa, na vinachukua muda mrefu sana kuwa navyo hawana.
Mtu
Anakosa uaminifu, heshima, uelewa, utayari wa kumsikiliza mwenzake, muda wa kuwa na mwenzake, mapenzi, kumjali kihisia na kimwili, kuona umuhimu wa mwenzi wake, anamnyanyasa mwenzake kimwili/kihisia na kifikra, hajishughulishi jikoni, sebleni wala chumbani (kwa wamama zaidi. . kila kitu dada wa kazi), anakua na dharau, anamtumia mume kifedha/kimwili, anamdharau mwenzake na kufidia hayo yote kwa kuwa na PESA, UMBO ama SURA NZURI.
Yani kwenye jamii yetu kumpata mwenye pesa ni rahisi kuliko kumpata mtu ambae ana"strong values" "good morals" na ni "well mannered". Na ukisema unatafuta mwenzi wa aina hiyo watu watakushangaa kuliko ukisema unatafuta mtu wa kumchuna a.k.a ATM , tena zinazotembea. . lolz.
Swali : WEWE ukiambiwa uchague kati ya 'sura nzuri, pesa, umbo la kupindisha shingo za wake kwa waume' na ' stong values, good manners, good morals' utachagua kipi?