FIFA Compliance Head Says Russia, Qatar World Cups Could Be Taken Away

FIFA Compliance Head Says Russia, Qatar World Cups Could Be Taken Away

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
FIFA Compliance Head Says Russia, Qatar World Cups Could Be Taken Away

ZURICH — Russia and Qatar could be stripped of their World Cup hosting rights if evidence emerges of bribery in the bidding process, the independent chairman of FIFA's audit and compliance committee told a Swiss newspaper.

The FBI's investigation of bribery and corruption at FIFA includes scrutiny of how soccer's governing body awarded World Cup hosting rights to Russia and Qatar, a U.S. law enforcement official told Reuters this week.
Domenico Scala told SonntagsZeitung that FIFA the two countries could lose the hosting rights should evidence emerge of bribery in the bidding process.


Russia's President Vladimir Putin (R) and FIFA President Sepp Blatter take part in the official hand over ceremony for the 2018 World Cup scheduled to take place in Russia, in Rio de Janeiro in this July 13, 2014 file photo. RIA NOVOSTI / Reuters
"If evidence should emerge that the awards to Qatar and Russia only came about thanks to bought votes, then the awards could be invalidated," Scala said in an interview published on Sunday. "This evidence has not yet been brought forth."
Russia and Qatar have previously denied wrongdoing in the conduct of their bids for the 2018 and 2022 tournaments, which were not the subject of charges announced by U.S. prosecutors last week against FIFA officials.
Scala had made similar comments in 2013 but events over the last two weeks, which included a dawn police raid in Zurich and the arrests of several FIFA officials on U.S. charges, have added urgency to his remarks.
Sepp Blatter unexpectedly announced on Tuesday he was resigning, just four days after securing a fifth term as FIFA president and shortly before it emerged that he too was under investigation by U.S. law enforcement.

In a separate interview with Swiss paper Sonntags Blick, Scala also floated the idea of term limits for the FIFA presidency.
"If a FIFA president does two or three cycles that is enough," Scala is quoted as saying.
A representative for Scala confirmed his remarks.
FIFA did not immediately respond to a request for comment.

 
Na hayo maandalizi waliongia itakuwaje.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Na hili ndilo linaweza kusababisha mpasuko mkubwa wa FIFA kama tuijuavyo hivi leo. Russia na Qatar pamoja nchi nyingi za East Europe na Middle East zitakuja juu kwa kudai Marekani na UK wanataka kuwapokonya Russia na Qatar haki waliyopewa na FIFA na ambayo wameshaingia gharama za mabilioni ili kujiandaa na mashindano ya Kombe la Dunia 2018 na 2022. Kama hekima na busara havitatumika ili kutoisambaratisha FIFA basi kombe la dunia la mwisho linaweza kabisa kuwa lile lililofanyika Brazil 2014.

Na hayo maandalizi waliongia itakuwaje.
 
Na hili ndilo linaweza kusababisha mpasuko mkubwa wa FIFA kama tuijuavyo hivi leo. Russia na Qatar pamoja nchi nyingi za East Europe na Middle East zitakuja juu kwa kudai Marekani na UK wanataka kuwapokonya Russia na Qatar haki waliyopewa na FIFA na ambayo wameshaingia gharama za mabilioni ili kujiandaa na mashindano ya Kombe la Dunia 2018 na 2022. Kama hekima na busara havitatumika ili kutoisambaratisha FIFA basi kombe la dunia la mwisho linaweza kabisa kuwa lile lililofanyika Brazil 2014.

Busara na hekima ni kufuata sheria na taratibu husika ili kuwe na haki pande zote, kama ikigundulika zilikiukwa katika kuwapatia hao jamaa haki za kuandaa hiyo michuano tena kwa makusudi, then hakuna mjadala. Hata kama itamaanisha kuivunja FIFA, na iwe tu.
 
Na hili ndilo linaweza kusababisha mpasuko mkubwa wa FIFA kama tuijuavyo hivi leo. Russia na Qatar pamoja nchi nyingi za East Europe na Middle East zitakuja juu kwa kudai Marekani na UK wanataka kuwapokonya Russia na Qatar haki waliyopewa na FIFA na ambayo wameshaingia gharama za mabilioni ili kujiandaa na mashindano ya Kombe la Dunia 2018 na 2022. Kama hekima na busara havitatumika ili kutoisambaratisha FIFA basi kombe la dunia la mwisho linaweza kabisa kuwa lile lililofanyika Brazil 2014.

Tuombe hilo lisitokee ama ndio utakuwa mwisho wa fifa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kulikuwa na usanii mkubwa ulikuwa unaendelea FIFA,kuna scandal nyingine kuwa Morocco ndio walipaswa kuandaa WC 2010 South Africa wakahonga waandae wao
 
pic+blateer.jpg

Sepp Blatter.
Na Mwandishi wetu

Posted Jumatatu,Juni8 2015 saa 14:4 PM
Kwa ufupi
Zilikuwa ni fainali za Dunia jina, kwani wakati huo fainali hizo zilikuwa na timu nyingi za Ulaya na Amerika, huku mabara ya Afrika na Asia yakiwakilishwa na timu moja kila moja.

Mwaka 1966, Shirikisho la Soka Afrika (Fifa), lilikuwa linaongozwa na raia wa England, Stanley Rous na mwaka huo England ndiyo ilitwaa ubingwa wa dunia.

Zilikuwa ni fainali za Dunia jina, kwani wakati huo fainali hizo zilikuwa na timu nyingi za Ulaya na Amerika, huku mabara ya Afrika na Asia yakiwakilishwa na timu moja kila moja.

Katikati ya miaka ya 1970, nchi nyingi za Afrika na Asia zilikuwa zimepata uhuru na nyingi zilikuwa zimepata uhuru kutoka kwa Mwingereza na zilianza kupata sauti. Fifa wakati huo ilikuwa kama sehemu ya mamlaka ya ukoloni na ilikuwa ikifahamika kwamba inaunga mkono serikali ya ubaguzi wa rangi ya Afrika Kusini.

Mwaka 1974, mwanasheria kutoka Brazil, Joao Havelange alimshinda Rous katika uchaguzi na hivyo kuwa Rais mpya wa Fifa na ndipo alipoanza kufanya mageuzi makubwa ndani ya Fifa.

Havelange alisaidia kuongeza idadi ya timu katika Fainali za Kombe la Dunia kutoka timu 16 hadi 32 na hivyo kuongeza idadi ya timu nyingi za Afrika na Asia kushiriki katika fainali hizo. Pia alianzisha mashindano ya dunia ya vijana kwa umri tofauti na kuifanya Fifa kuwa shirika kubwa linaloongoza mchezo wa soka.

Mwaka 1998 akiwa na miaka 82 aliacha kuiongoza Fifa na kumpendekeza Sepp Blatter (raia wa Uswisi) kuwa ndiye anafaa kuliongoza Shirikisho hilo. Wakati huo Blatter alikuwa katibu mkuu wa Fifa. Wakati huo huo, Ulaya ya Kaskazini ilikuwa ina mpango wa kutaka kupata tena nafasi ya kuiongoza Fifa, kwa hiyo ilikuwa ikiona Rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa), Lennart Johansson ndiye anayefaa kuiongoza Fifa, lakini alishindwa na Blatter.

Kushindwa kwa Johansson kulichangiwa pia na kauli aliyoitoa baada ya kuja Afrika na kurudi Ulaya, alisema, "Nilipokwenda Afrika Kusini, chumba chote cha mkutano kilikuwa na watu weusi na kilikuwa na giza wakikaa chini kwa pamoja, jambo jingine hawana mzaha wanapokasirika kwa hiyo nilikuwa nikifikiria kwamba itakuwaje watakapokasirika."

Kauli hiyo iliwaudhi viongozi wa soka wa Afrika kwa hiyo kura zao walimpa Blatter.

Blatter ambaye alishinda uchaguzi huo kirahisi, aliamua kuvunja utawala wa Ulaya na Amerika katika kuandaa Fainali za Kombe la Dunia na kuipa Japan na Korea Kusini kuandaa Fainali za Kombe la Dunia 2002.

Hata hivyo, ugomvi wa Blatter na nchi za Ulaya ulianza alipotangaza kuwa anataka kuzipeleka Fainali za Kombe la Dunia barani Afrika na alikaribia kuzipeleka mwaka 2006. Hata hivyo, mjumbe wa Bara la Oceania, Charlie Dempsey alijitoa katika dakika za mwisho za upigaji kura, hivyo Ujerumani ikaishinda Afrika Kusini.

Baada ya hapo Blatter alikuja na mpango kwamba Fainali za Kombe la Dunia zifanyike kwa mzunguko katika mabara yote. Kwa hiyo Fainali za Kombe la Dunia za 2010 alichagua zifanyike Afrika. Kura zikapigwa kati ya Morocco na Afrika Kusini ambayo iliibuka mshindi.


Miaka michache baada ya kura hizo kupigwa, vyombo vya habari vya England vikaanza kutoa habari mbaya kuhusu Afrika Kusini vikionyesha kwamba nchi hiyo ina uhalifu wa hali ya juu. Matukio ya ubakaji na mauaji mengi.

Pia vilitangaza kwamba viwanja havitakamilika kabla ya mashindano, watu wengi wanaishi kwenye makazi yasiyo rasmi na viliwahoji baadhi ya watu wa Afrika Kusini ambao walikuwa wakiiponda nchi yao kwa kuwekeza fedha nyingi katika fainali hizo badala ya kuzitumia katika sekta ya elimu.

Vyombo hivyo vya habari pia vilianza kuchagua nchi ambazo zitafaa kuandaa fainali hizo kwa madai kuwa Afrika Kusini inaonekana haiwezi na waliitaja England ndiyo inayofaa na nafasi ya pili wakaipa Ujerumani.

Kabla ya kufanyika kwa Fainali za Kombe la Dunia, hufanyika mashindano ya mabara ambayo yalifanyika Afrika Kusini mwaka 2009 kwa mafanikio.


Pia, kabla ya kufanyika kwa Fainali za Kombe la Dunia, huwa inapangwa ratiba, dakika chache kabla matangazo ya televisheni hayajaanza, mpiga picha kutoka Ujerumani aliweka begi ndani ya ukumbi na kupiga kelele za bomu akitaka watu wakimbie, lakini polisi waliwatuliza na polisi mmoja alilifuata begi lile na kukuta ndani yake kuna vitabu tu. Siku zote kama kuna bomu ndani ya jengo ina maana watu wote huondolewa ili kuwapisha askari ambao ni wataalamu wa mabomu ili kuliondoa, hiyo ina maana matangazo ya moja kwa moja yangechelewa na hivyo nchi za Ulaya zingesema Afrika bado haina uwezo wa kuandaa fainali hizo.

Baada ya Fainali za Kombe la Dunia 2010 kumalizika nchini Afrika Kusini, Rais wa klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani, Uli Hoeness alisema uamuzi wa Fifa kuzipeleka fainali hizo Afrika ulikuwa wa makosa na kudai kuwa uamuzi huo ulifanyika kwa rushwa.


Hata hivyo, Blatter alimjibu Hoeness kwa kusema, "Kuna ule mtazamo wa kizamani kwa nchi za Ulaya kwamba kwa nini Afrika iandae Fainali za Kombe la Dunia, unajua wakoloni kwa zaidi ya miaka 100 walienda Afrika na kuchukua vitu vyao vizuri vingi na mpaka sasa wanachukua wachezaji wao bora, hakuna heshima kabisa."


Baada ya Afrika kupewa nafasi ya kuandaa fainali za 2010, fainali hizo zilipelekwa Amerika Kusini na Brazil iliziandaa 2014. Baada ya hapo fainali hizo zilitakiwa kufanyika Ulaya, hivyo England ilikuwa ikiona ina nafasi kubwa ya kuandaa fainali za 2018, lakini ikapewa Urusi.

Baada ya England kushindwa ndipo walipoibuka kwa nguvu kubwa kwamba Fifa imejaa rushwa na kufanya kampeni za kumwangusha katika uchaguzi wa 2015. Hata hivyo alishinda, lakini siku chache baada ya ushindi huo aliamua kutangaza kujiuzulu baada ya kuona nchi za Ulaya zinampinga.


Sawa, Blatter anaondoka atakuja kiongozi mwingine, lakini ukiacha kuzileta fainali za dunia barani Afrika, Blatter ndiye alifanya klabu za Afrika ziingie katika mashindano ya dunia ya klabu.

Kwani awali mashindano hayo yalishirikisha klabu za Ulaya na Amerika ya Kusini. Blatter pia ndiye aliyeanzisha mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.

Blatter ndiye aliyeanzisha mpango wa kutoa fedha sawa kwa mashirikisho yote ya soka duniani baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia.

Fedha hizo zimekuwa msaada mkubwa kwa maendeleo ya mashirikisho mbalimbali ya soka ya nchi za Afrika.

Baada ya kumalizika kwa fainali za 2014, kila shirikisho lilipewa Dola 750,000 za Marekani.

Blatter alianzisha utaratibu wa kulipatia kila shirikisho la soka Dola 250,000 za Marekani kila mwaka.

Baada ya Fainali za Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini, Blatter aliziongeza na kuanzisha miradi mingi kwa ajili ya kusaidia soka la Afrika. Kwa mfano, ulianzishwa mradi wa ‘Win in Africa with Africa' ukiwa na bajeti ya zaidi ya Dola 39 milioni kwa ajili ya kutengeneza viwanja (sehemu ya kuchezea) katika nchi 52 za Afrika.

Blatter alianzisha pia mradi wa ‘Goal' wenye lengo la kusaidia miradi mbalimbali ya soka Afrika hasa miundombinu kama sehemu za kuchezea, vifaa, malazi na vituo vya ufundi, mradi huu hufanyika pale Shirikisho husika linapoomba fedha Fifa.

Blatter hakuishia hapo, kwani alianzisha mradi wa ‘Football for Hope' na kujenga vituo mbalimbali barani Afrika vyenye viwanja vya soka ili watoto au vijana walio na maambukizi ya Ukimwi, mazingira magumu au nchi iliyokosa amani na majanga mengine waweze kucheza mpira wa soka.

Alihakikisha Fifa inaendesha kozi mbalimbali za makocha, waamuzi, utabibu na utawala kwa lengo la kuhakikisha mafunzo hayo yanasaidia maendeleo ya soka la Afrika.

Kwa ujumla, kwa mujibu wa Fifa, toka mwaka 1999, shirikisho hilo likiwa chini ya Blatter, limetoa zaidi ya Dola 500 milioni za Marekani kwa ajili ya maendeleo ya soka la Afrika.


Ndiyo maana kuondoka kwa Blatter kutakuwa pigo na pengo kubwa kwa Afrika kwani aliipigania ndiyo maana uchaguzi uliopita alipata kura 54 za nchi za Afrika.


 
Changa la macho... Hii yote ni siasa kati ya West vs East. Baada ya miaka 10 au baada ya utawala wa Putin mtakuja kusikia ukweli wa hii skendo (kama vile tulivyojua sababu za kuuliwa kwa Ghadafi, kupinduliwa kwa utawala wa --------- miaka ya 1980, kuuliwa kwa Patrice Lumumba, majaribio ya kutaka kumuua Castro by JFK etc). FBI/Marekani wanajaribu kufichaficha lengo lao kwa kutundika vitanzi nchi nyingine (France, Sauzi, Qatar) wakati mlengwa tunamjua. Kitu kingine kwa nini hatusikii kwa sana rushwa iliyotolewa na France ili wa-host 1998? Vyombo vya habari vya ughaibuni vinang'ang'ania rushwa ya Sauzi, Russia na Qatar pekee yake wakati Ufaransa nayo imetajwa. Na kwa nini FBI(Marekani) hawatuambii walitoa rushwa kiasi gani ili Marekani ipate 1994 hosting rights? Ina maana rushwa ndani ya FIFA ilianza 1998? Bottom line hii ni A WAY TO PUNISH PUTIN/RUSSIA.
 
Russia hawastahili kuaandaa mashindano haya kwasababu:

1. Russia is the worst culprit katika ukiukaji wa haki za kibinadamu
2. Russia is the worst culprit katika ubaguzi wa rangi --> Ukiwa mweusi, go there for the world cup at your own risk
3. Russia bullies and destabilizes its neighbors.

If Russia and Qatar leave FIFA, few will be sad. All of Russia's neighbours will cheer.
 
Back
Top Bottom