FIFA kuidhinisha programu ya kuripoti upangaji wa matokeo ya mechi kabla ya mchezo husika

FIFA kuidhinisha programu ya kuripoti upangaji wa matokeo ya mechi kabla ya mchezo husika

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105
Bodi ya uongozaji mpira wa miguu duniani FIFA imeidhinisha programu nukushi (App) iliyotengenezwa mahususi ili kusaidia wachezaji kuripoti vitendo vya kupanga matokeo kabla ya mchezo.

Programu yenye kitufe chekundu, ambayo inamilikiwa na umoja wa wachezaji duniani (FIFPRO) itasambazwa kwa wachezaji duniani kote kupitia umoja wa nchi husika kama vile Professional Football Association(PFA ) ya Uingereza.

Itatumika kusaidia kifaa cha kuripotia ambacho kilikuwepo kabla kilichowekwa na FIFA.Taarifa zitakazo pokelewa kupitia Programu nukushi (App) hiyo zitafanyiwa uchunguzi na bodi inayosimamia uadilifu.

Shirika la umoja wa ulaya linalojihusisha na maswala ya sheria limesema kuwa mpira wa miguu ni mchezo ambao unalengwa zaidi na wahalifu kupitia kwenye kupanga matokeo kabla ya mchezo.

Mkurugenzi wa maswala ya kisheria wa FIFPRO Roy Vermeer amesema “ tuna uhakika hili litaimarisha mkono wa mpira wa miguu na mamlaka za umma kwenye kupambana na vitendo vya upangaji wa matokeo kabla ya mchezo kuchezwa.”

“Kufuatia wachezaji kukumbana na hatua za kinidhamu kwa kushindwa kutoa taarifa za upangwaji wa matokeo kabla ya michezo, lazima kuwe na njia ya wao kuweza kufanya bila kuhofia kujiingiza wao, familia zao pamoja na taaluma zao matatani" aliongeza Vermeer.

Inaelezwa kuwa vitendo vya upangaji wa matokeo kabla ya mchezo husika hufanywa ili kuwanufaisha watu wanaoshiriki bahati nasibu.

CHANZO: FIFA approves app for players to report match-fixing approaches
 
Aisee, Naionea huruma Timu ya wananchi.
Kuna wakati goli linaingia golini kwao halafu refa anasema hiyo ni kona.
 
Back
Top Bottom