FIFA kupiga kura kuruhusu sub nne

Ochutz

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2011
Posts
465
Reaction score
106
Bodi ya FIFA inayosimamia sheria za mpira wa miguu duniani inakutana kwa siku mbili kuanzia Ijumaa ili kufanya marekebisho muhimu ya sheria.

Bodi hiyo inakutana ikiwa na ajenda kuu mbili, ya kwanza ni kupiga kura iwapo iruhusu timu kufanya mabadiliko hadi wachezaji wanne kwa michuano ya mtoano inayochezwa zaidi ya dakika tisini.


Pili kuwapa fursa makocha kupata taarifa za mfumo wa digitali unaotunza kumbukumbu za wachezaji wanapokuwa uwanjani ili kuweza kufahamu ni mchezaji yupi amechoka na inaweza kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi wanapofanya sub.


Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtandao wa GOAL, iwapo kanuni hiyo itarekebishwa, basi itawanufaisha zaidi Kocha wa Chelsea Jose Mourinho na Carlo Ancelotti kocha wa Real Madrid ambao ndio wanaamika kuwa wataalamu sana wa kubadilisha matokeo ya mchezo kwa kutumia wachezaji wanaotoka benchi.

Chanzo: TikTak
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…