shaks001
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 1,246
- 1,070
Nimeshtushwa sana na taarifa hii kutoka makao makuu ya soka duniani, Fifa kuwa itasitisha misaada mingine ya kimaendeleo ya soka kwa Tanzania kisa tu serikali kuzuia vifaa vya michezo zikiwemo nyasi bandia za uwanja wa Nyamagana, Mwanza.
Hii ni kutokana na kodi serikali iliyotoza kwenye nyasi hizo bandia na kupelekea nyasi hizo kukaa bandarini kwa zaidi ya mwaka sasa.
Najaribu kujiuliza,inakuwaje Serikali hii hii inayojinasibu kuwa inataka kuinua michezo nchini hususani soka kushindwa kusamehe kodi vifaa hivyo ili hawa mabosi wa soka wasije kusitisha misaada yao katika maendeleo ya soka letu?
Ikumbukwe pia kuna mpango wa Fifa wa kuendeleza uwanja wa Gombani, Pemba na ule wa Karume jijini Dar.
Ushauri wangu kwa Serikali: Sisi wapenda soka haturidhishwi na kiwango cha soka letu mpaka sasa, inapotokea watu wadau wanataka kututoa tulipo na kutupeleka hatua nyingine ya juu, nanyi mnaturudisha nyuma; hatutawaelewa!
Jaribuni kutatua mzozo huu tuendelee na mengine.
Chanzo: StarTV Habari