FIFA kuwalipa wachezaji ambao hawapati mishahara klabuni

DullyJr

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
13,983
Reaction score
11,857

Shirikisho la Soka Duniani FIFA na umoja wa wachezaji FIFPRO unaandaa mfuko utakaosaidia kuwalipa wachezaji wasio na mishahara na wale ambao hawapati mishahara pindi klabu zao zinapopitia changamoto za kiuchumi.

Hiyo imekuja kufuatia muendelezo wa klabu nyingi duniani kuporomoka kiuchumi, ambapo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, jumla ya klabu 20 duniani zimeanguka kiuchumi na kukwamisha mamia ya wachezaji.

Mfuko huo utazisaidia kulipa mishahara klabu klabu zilizoporomoka kiuchumi huku zikiwa zinafanya biashara ili zirejee katika hali yake.

Rais wa FIFA, Gianni Infantino amesema ametenga kiasi cha Pauni Milioni 12.3 kwa ajili ya kuwasaidia wachezaji ambao hawatalipwa na klabu zao kuanzia 2020 hadi 2022 huku takribani Pauni Milioni 3.8 zikitengwa kuwalipa wachezaji ambao hawajalipwa kuanzia 2015 hadi 2020.

"Makubaliano kati yetu na washirika wetu ni kuwasaidia wachezaji walio katika mazingira magumu na kazi yetu ni kuonesha uwepo wetu kama chombo kinachoongoza mpira", amesema Infantino.


Nina wasiwasi Yanga wataukomba mfuko wte

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waje tz haraka sana maana klabu zinazolipa mishahara ni mbili tu
 
Wasiishie kwenye vilabu na wachezaji pekee!

Kuna timu za taifa zimeshindwa kulipa posho kwenye michuano ya kimataifa.

Kuna makocha wa vilabu na timu za taifa pia ni wahanga wa timu kuporomoka kiuchumi.
 
Suala zuri ila naomba please wasianzie Tanzania pleasea please

Majimaji fc account 0.04 %Tsh

Stand united account 000.7% Tsh

Yaani zipo nyingi ambazo account zao zinasoma frequency za redio
 
Suala zuri ila naomba please wasianzie Tanzania pleasea please

Majimaji fc account 0.04 %Tsh

Stand united account 000.7% Tsh

Yaani zipo nyingi ambazo account zao zinasoma frequency za redio
Wewe ya kwako inasoma shingapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…