FBI kwa sasa inachunguza hela za rushwa ambazo viongozi wa FIFA walilipwa ama na mashirika ya kimarekani, yenye uhusiano na Marekani au pesa za rushwa walizolipwa viongozi wa fifa zilizopitia bank za marekani. Pia kama kuna raia yoyote wa Marekani aliyeshiriki Katika kupokea, kutoa au kutakatisha pesa za rushwa zinazohusiana na fifa
Hii ni baada ya kumfuatilia jamaa mmoja Mmarekani kwa muda wa miaka kadhaa na kugundua alikuwa ana husika na kufanya deal za rushwa na viongozi wa bodi ya fifa na huyo jamaa baada ya kubanwa aliwauza wenzake wakati wa kupiga kura za world cup 2018 na 2022 ambapo baadhi walichukua hela kutoka Russia na Quatar bila kujua FBI wametegesha