FIFA na habari ya viwanja kupewa jina la Pele

FIFA na habari ya viwanja kupewa jina la Pele

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Ndio Rest in eternal peace Pele mchawi wa soka japo sikupata kukushuhudia ukicheza hakika dunia imepoteza wakali wa mpira Maradona na Pele.

Pia ni funzo kwa sisi tuliobaki tujue tupo safarini pamoja na fujo zote za maisha tukumbuke kuna futi 6 zinatungoja.

Twende kwenye Mada baada ya kifo cha Pele alisikika rais wa Fifa akitoa mawazo akisema ingependeza angalau kila nchi ingekipa kiwanja kimoja jina la Pele ila kumuenzi mkali huyo wa kabumbu kutoka nchi ya vipaji Brazili

Ndio ni wazo zuri ila Fifa kama taasisi kubwa ya mpira ingekuja na pendekezo kama hili kwa zile nchi zenye viwanja vingi sawa watafute kiwanja kimoja wakiiite Pele.

Ila kwa nchi zinazoendelea mfano kama nchi yetu Ingependeza kama FIFA WANGETOA PESA KWA AJILI YA UJENZI WA VIWANJA VIPYA NA KUVIPA JINA LA PELE NAHISI KILA NCHI MWANACHAMA ANAPEWA FUNGU LA FIFA BASI NI VEMA WANGEELEKEZA FEDHA HIZO ZIJENGE HIVYO VIWANJA.

Hakika hapo ndio ingekua mchango sahihi wa kumuenzi Hayati Pele.
 
Back
Top Bottom